Habari za Punde

Madiwani wa CCM watakiwa kutekeleza sera ya Ilani ya chama

 NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.


Chama Cha Mapinduzi kimewataka madiwani wake kuhakikisha wanatekeleza sera na ilani ya Chama hicho kwa kuwa mstari wa mbele kutatua kero zinazowakabili wananchi.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organization Zanzibar Bw Casian Galon Nyimbo ametoa kauli hilo alipokuwa akizungumza na madiwani baada ya kumaliza shughuli za uchaguzi Wa kumchagua Mwenyekiti wa Baraza la Mji Wilaya ya Kaskazi uliofanyika ofisi ya CCM wilaya hiyo huko Mahonda.

Bw. Galos amesema  dhamana walizokabidhiwa madiwani hao ni kwa ajili ya kutatua kero za Wanchi katika maeneo yao kwa kuzingatia kuwa wananchi wana matarajio makubwa kutokana na ahadi zilizotolewa na wagombea wa ngazi mbali mbali wa CCM wakati wa uchaguzi

Amesema  dhamira ya ccm ni kuona Ahadi za wagombea zinatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati ili wananchi wazidi kuwa na imani na chama hicho.

Naye Katibu wa Ccm Wilaya ya Kaskazini B Bi  Mwansiti Hassan Mohamed amewaasa madiwani hao kuweka mbele maslahi  ya  Chama na kuibua miradi itakayokuwa na manufaa na wananchi.

Naye Mwenyekiti mpya wa Baraza La Mji Kaskazini B bw. Hassan Ameir Abdalla ameahidi kushirikiana naviongozi wenzake ktika kuwatumikia wananchi kwa mujibu wa matatizo yao.

Amewaasa madiwani wenye tabia ya kutoa siri za vikao kuacha tabia hiyo kwa haina maslahi na Chama cha Malinduzi hasa wakati huu wa kuleta mageuzi ya kiuchumi.

Katika uchaguzi  bw Hassan Ameir Abdalla amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mji Kaskazini B na bibi Pili Mohamed Saidi amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyeliti

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.