Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Yafanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dr. Khalid Salum Mohamed Kushoto akimpokea na kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla kuhitimisha Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani hapo Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.
Vijana wa Jumuiya ya Kupambana dhidi ya Kuenea kwa Virusi vya Ukimwi Zanzibar ZAPHA+ wakiwasilisha ujumbe Maalum kupitia fani ya Mashairi kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani wakisimama wakati wa Wimbo Maalum wa Mashujaa hapo Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla akipokea Risala Maalum kutoka kwa Kijana Suhaila Msham wa Jumuiya ya Kupambana dhidi ya Kuenea kwa Virusi vya Ukimwi Zanzibar ZAPHA+ .
 Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ukimwi Zanzibar Dr.Salhia Ali Muhsin akitoa Taarifa ya hali ya Ukimwi Zanzibar kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dr. Khalid Salum Mohamed akitoa salamu kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Siku ya Ukimwi.
Baadhi ya Watendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar wakifuatilia baadhi ya matukio yaliyojiri kwenye Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakili wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
Baadhi ya Masheha wa shehia mbali mbali Nchini walioshiuriki Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani hapo Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.