Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais, Mhe Hemed akutana na Wafanyakazi wa Shirika la Bandari Zanzibar kusikiliza kero zao

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akiuagiza Uongozi wa Shirika la Bandari kuhakikisha kwamba haki za Wafanyakazi wake zinatolewa zote na kwa wakati ili kuleta ufanisi katika utendaji wa Shirika hilo.
 Bwana Saleh Yussuf Saleh wa Kitengo cha Uendeshaji ndani ya Shirika la Bandari akielezea changamoto zinazowapata ambazo zimekuwa zikizorotesha kasi ya uwajibikaji.
 Mzee Pangaras Manyipa Dereva wa Shirika la Bandari aliomba Mamlaka ya KuzuiaRushwa na uhujumu Uchumi {ZAECA} kufanya uchunguzi ili kubaini baadhi ya vitendo vya ukiukwaji wa Haki za Wafanyakazi ndani ya Shirika hilo.

Said Mohamed Abdullah akithibitisha ubinafsi unaofanywa na baadhi ya Viongozi wa Shirika la Bandari na kuviza kasi ya uwajibikaji kwa Watendaji wa Shirika hilo.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amesema ameamua kuhamia Bandari Kuu ya Malindi ili kuhakikisha mapato ya Taifa yanayokusanywa kutokana na eneo hilo muhimu ambalo ni lango Kuu la Uchumi yanakuwa salama.

Alisema kuanzia sasa Fedha ya Serikali lazima iheshimiwe ambapo Mtendaji wa Umma analazimika kujitathmini kama mkakati za Serikali katika kudhibiti mapato yake anaweza kwenda nao sambamba.

Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema hayo baada ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili Wafanyakazi wa Shirika la Bandari Zanzibar waliomuomba wakutane nae alipofanya ziara ya ghafla hapo juzi na kuahidi kutekeleza ombi lao.

Alisema wakati bandari inalazimika ifanye vyema katika kuiongezea Mapato Serikali Kuu Uongozi wa Shirika la Bandari una wajibu wa kuhakikisha Haki za Watendaji wake ikiwemo maposho ya muda wa ziara yanatolewa na kulipwa kwa wakati kwa lengo la kuongeza ari na nguvu zinakazohamashsiah  lango hilo la Uchumi wa Nchi linaimarika Zaidi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kwamba katika kuona ufanisi wa Kazi za Bandari unaongezeka Uongozi wa Shirika hilo utalazimika kutoa ripoti ya changamoto zilizopatiwa ufumbuzi ndani ya kipindi cha Mwezi Mmoja ifikapo Tarehe 30 Januari Mwaka 2021.

Mheshimiwa Hemed Suleiman alieleza kwamba kinachohitajika kwa Viongozi na Watendaji wa Shirika hilo ni kuendelea kushirikiana ipasavyo na kuepuka ubinafsi unaojenga kiburi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar kulifanyia kazi agizo la Rais kwa kupita katika katika Vitengo mbali mbali vya Shirika hilo ili kuelewa changamoto zinazowakabili.

Alisema pale atakapobaini yupo Mtendaji anashindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Kanuni, Taratibu na Sheria za Utumishi wa Umma Serikali ana haki na wajibu wa kumchukulia hatua, vyenginevyo wimbi hilo litamuelekea yeye mwenyewe.

Wakitoa malalamiko yao Wafanyakazi wa Vitengo mbali mbali vya Shirika la Bandari walimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ucheleweshwaji wa malimbikizo yao ya posho umekuwa ukipunguza ari yao ya uwajibikaji.

Wafanyakazi hao waliomba pia kupatiwa mafunzo kwa lengo la kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi sambamba na upatikana wa bima ya afya kwa wakati.

Mapema Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mheshimiwa  Rahma Kassim Ali  aliahidi kwamba ule Muundo wa shirika la Bandari ambao umetengenezwa kwa kushirikisha wawakilishi wa vitengo vyote ambao umesharidhiwa na Serikali Kuu ataufuatilia kwa ajili ya kuanza kufanya kazi. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.