Habari za Punde

Mwakilishi wa Mwera awataka Wanachama wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar kushirikiana na serikali

Na Takdir Suweid Zanzibar                           5.12.2020.

 

Mwakilishi wa Jimbo la Mwera Mihayo Juma Nunga amewataka Viongozi na Wanachama wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar  kushirikiana na Serikali ya awamu ya nane katika kupiga vita vitendo vya udhalilishaji kwa Wanawake na Watoto.

 

Amesema Serikali imeweka maazimio ya kuwalinda Wanawake na Watoto kwa kuondosha udhalilishaji,ubakaji,Utoro katika Skuli na Utumiaji wa Dawa za kulevya hivyo ni vyema kuiunga Mkono ili azma hiyo iweze kufikiwa.

 

Ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharibi B wakati alipokuwa akifunguwa Mkutano wa 4 wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA),ilioambatana na Uchaguzi Mkuu.

 

Amesema katika kuelekea uchumi Buluu kuna fursa nyingi ikiwemo za kilimo,uvuvi,Ufugaji na Biashara hivyo ni vyema kwa Viongozi wa Jumuiya hiyo kuweka mikakati ya kuzifikia fursa hizo ili ziweze kuwasaidia Wanawake na Watoto kwa kupata maendeleo na kufikia azma ya Serikali kufikia Uchumi wa Bluu.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Tauhida Cassian Galos amesema lengo la kuanzisha Jumuiya hiyo ni kuwasaidia kuondosha tatatizo la Udhalilishaji katika jamii,kuwawezesha Wanawake,Watoto na Wenyeulemavu ili waweze kupata maendeleo na kuiomba jamii kushirikiana ili kufikia malengo yaliokusudiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.