RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Jijini Zanzibar Askofu Michael Hafidh, alipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi huo leo 26-1-2021.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Jijini Zanzibar Askofu Michael Hafidh (kulia kwa Rais) akiwa na ujumbe wake Ndg.Edwin Mkwaya na Ndg.Luis Majaliwa, walipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana Jijini Zanzibar Askofu Michael Hafidh baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibaer na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
Rais Dk. Mwinyi
alikutana na Baba Askofu Michael Henry Hafidh ambapo katika maelezo yake alimpongeza
Askofu huyo pamoja na Waumini wote wa Kanisa la Anglikana kwa kuendelea
kuiombea nchi amani.
Pamoja na hayo, Rais
Dk. Mwinyi alizipongeza juhudi za uongozi wa Kanisa hilo la kutaka kujenga Chuo
cha Amali huko kisiwani Pemba pamoja na azma yao ya kutaka kuekeza katika eneo
la Kiungani Jijini Zanzibar.
Mapema Baba Askofu
alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa ushindi mkubwa alioupata na kueleza matumaini
makubwa waliyonayo wananchi wa Zanzibar kutokana na uongozi wake huku akimpongeza
kwa kuwepo kwa maridhiano na hatimae kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment