Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais asaini kitabu cha maombolezo kifo cha cha aliekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abadalla akisaini kitabu cha maombolezo kufutia kifo cha aliekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  na mwenykeiti wa chama cha ACT  Wazalendo Maali Seif Sharifu Hamad kilichotokea Febuari 17 mwaka huu jijini Dar es Salam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Na Kassim Abdi, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amefika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa AbdulWakil Kikwajuni kwa ajili ya kusaini kitabu cha Maombolezi kufufutia msiba wa aliekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharifu Hamad.

Makamu wa Pili wa Raisi amesaini kitabu hicho  kutokana na kifo cha Maalim seif  kilichotokea siku ya Jumatano ya tarehe 17/02/2021 majira ya saa Tano dakika ishirini na sita (5:26) katika hopital ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Maliim seif mnamo mwaka 1977-1980 aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na mjumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar.

Pia, Maalim Seif Sharifu Hamad kabla ya umauti kumfika amewahi kushika nyadhifa mbali mbali serikalini ikiwemo Waziri wa Elimu katika serikali ya Rais Aboud Jumbe mnamo miaka ya 1977- 1980 na baadae kushika wadhifa wa waziri kiongozi katika serikali ya Rais Sheikh Idrissa Abdulwakili Nombe.

Aidha, Maalim Seif amewahi kuwa Mjumbe wa kamati kuu na Mkuu wa idara ya uchumi na Fedha kupitia Chama cha Mapinduzi katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

Mnamo mwaka 1992 mara baada ya kuanzishwa kwa  mfumo wa vyama vingi Maalim Seif pamoja na wenzake, waliasisi chama na kuendeleza harakati za siasa nchini.

Maalim Seif amewahi Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF kwa miaka kadhaa na amewahi kugombea nafasi ya urasi wa Zanzibar kupitia chama hicho kwa miongo tofauti.

Maalim Seif Sharif Hamad amepata bahati ya kusaliwa katika viunga vya mskiti Maamuri uliopo mtaa wa Upanga jijini Dar es Salam na baadae maiti yake kufikishwa Unguja na kusaliwa katika viwanja vya maisara.

Katika siku hiyo ya Alhamis mwili wa marehemu Maliim Seif Sharif Hamad ulisafirishwa kisiwani Pemba na kusaliwa katika uwanja wa Gombani na hatimae kupelekwa kijijini kwao Mtambwe Nyali wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad atakumbukwa kwa moyo wake wa kujitolea katika kuhubiri na kuimaisha umoja wa kitaifa na kuhubiri Amani visiwani Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla.

Maalim Seif ameacha kizuka na watoto wane (04)

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Peponi Amiin.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.