Habari za Punde

Sekta Binafsi Zina Mchango Mkubwa Zikifanya Majukumu Yake.

Mkurugenzi idara ya uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Dkt,Haji Salim Khamis alipokua akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku tano katika ukumbi wa kidogo chekundu mjini Unguja.
Meneja mradi wa Viungo ofisi ya Unguja Amina Ussi Khamis akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa mabwana shamba na bibi shamba.
Miongoni mwa washiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo mabwana shamba na mabibi shamba mafunzo yaliolenga kuwajengea uwezo kuhusu utowaji wa huduma katika kilimo cha shamba darasa.

Na.Muhammed Khmis

Mkurugenzi Idara ya uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Dkt,Haji Salim Khamis amesema katika kukuza maendeleo ya Zanzibar  Sekta binafsi zina mchango mkubwa iwapo zitafanya majukumu yake inavyostahiki kwa maslahi ya umma.

Ameyasema hayo wakati alipiokua akifungua mafunzo ya siku tano kwa mabawana shamba na mabibi shamba yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuanda na kuratibu vyema shamba darasa kupitia wilaya tano za Unguja katika mradi wa Viungo uliofadhiliwa ja umoja wa Jumuia za Ulaya visiwani hapa.

Alisema wakati Serikali ikiendelea na jitihada zake za kukuza uchumi wa Zanzibar ni wazi kuwa wanategemea sana sekta binafsi kukuza ajira na kuongeza kipato kwa wananchi wake.

Pamoja na hayo alisema sekta ya kilimo ni miongoni mwa sekta muhimu Zanzibar hivyo  kila mmoja katika washiriki hao wa mafunzo wana wajibu wa kuhakikisha wanasikiliza na kuelewa vyema mafunzo hayo ili kuwanufaisha wengine katika jamii zao. 

Sambamba na hilo aliwataka watekelezaji wa mradi huo wa Viungo kuhakikisha wanasimamia vyema wajibu wao wakifahamu kuwa mategemeo makubwa ya Serikali kwa wananchi wake ni kupitia mradi huo.

Kwa upande wake Meneja mkuu wa mradi huo Amina Ussi Khamis aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa wabunifu mara watakapomaliza masomo yao ya siku tano.

‘’Nyinyi mtakaopata mafunzo haya ni matumaini yetu kuwa mtakwenda kuwa wabunifu na kuwa chachu ya mabadiliko katika maeneo yenu’’aliongezea.

Aidha alisema  utaratibu wa kuwapatia mafunzo mabwana shamba unalenga kuwafunza utaratibu mzuri wa shamba darasa ambayo yatatumiwa kuwafundisha wanufaika wa mradi huo wa viungo.

Alieleza kuwa kwa kuwa mradi huo ni wakilimo cha kisasa utajikita zaidi kwenye njia za kitalamu ambazo wahusika watalazimika kujifunza kilimo na kukielewa vyema kabla ya shughuli za utekelezaji wenyewe.

Miongoni mwa washiriki hao kutoka wilaya tano za Unguja walisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ukizingatia mahitaji ya wakulima wengi kwenye maeneo yao wanayofanyia kazi.

Mize Juma kutoka wilaya ya kusini Unguja alisema baadhi ya wakulima wanashindwa kufanya vizuri katika kilimo kutokana na kukosa elimu bora ambayo ingewawezesha kufanya shughuli zao kwa weledi mkubwa.

Alisema kupitia mafunzo hayo anaamini kuwa yatawajengea uwezo na kuwafanya wao kuwa weledi wazuri wa maswala ya kutunza na kuandaa shamba darasa.

Mradi huo wa Viungo unatekelezwa na TAMWA-Zanzibar,CFP,PDF chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) na unatekelezwa muwa wa miaka minne.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.