RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisaini kitabu cha maombolezi ya kifo cha
aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe
Magufuli,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam
leo 19-3-2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar es Salaam baada ya kusaini kitabu cha maombolezi cha Hayati
Dkt. John Pombe Magulili aliyekuwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi ametia saini kitabu cha maombolezi ya kifo cha aliyekuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Joseph Pombe Magufuli
aliyefariki dunia Machi 17, 2021.
Rais Dk. Mwinyi ametia saini kitabu hicho cha maombolezi huko katika viwanja vya ukumbi wa Karimjee, ulioko Jijini Dar es Salaam na kueleza jinsi alivyopokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha kiongozi huyo.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza jinsi Hayati Rais Magufuli alivyoitumia nchi kwa nidhamu kubwa sana ikiwa ni pamoja na kusimamia kiuchumi na kimaendeleo kwa misingi ya amani, utulivu, umojana mshikamao.
Mapema Rais Dk. Mwinyi alimfariji na kumpa pole Mjane wa Hayati Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Dk. Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi walimpa pole Mjane wa Marehemu Hayati Magufuli Mama Janet Magufuli na kumtaka awe na subira yeye pamoja na familia yake katika kipindi hichi kigumu cha msiba.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment