Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amefanya Ziara Kutembelea Ujenzi wa Soko la Muda la Wafanyabiashara Kibanda Maiti leo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Kibanda Maiti akisalimiana na Viongozi akiwa katika ziara yake kukagua maendeleo ya ujenzi wa eneo la Soko la muda la Wafanyabiashara ndogondogo aliloliangiza kujengwa katika eneo hilo kwa ajili ya Wafanyabishara hao.

Munekano wa mabanda ya Soko la Muda la Wafanyabishara ndogondogo yakiwa katika hatua ya mwisho ya ujenzi wake kwa ajili ya matumizi ya Biashara.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana (kushoto kwa Rais) wakati akitembelea Soko la muda la  Wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la Kibanda Maiti akiwa katika ziara yake kutembelea Soko hilo linaloendelea na ujenzi wake na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mhe.Masoud Ali Mohammed,Waziri wa Maji na Nishati Mhe. Suleiman Masoud Makame na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa akitoa maelezo ya ujenzi wa mabanda ya wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la Kibanda maiti Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake kutembelea eneo hilo kujionea maendeleo ya ujenzi huo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi na Wafanyabiashara wa eneo la Kijangwani wanaotakiwa kuhamia katika eneo hilo la kibanda maiti kufanya biashara zao, akiwa katika ziara yake kutembelea ujenzi huo.
WANANCHI wa enao la mikunguni na Wafanyabiashara wa eneo la Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wananchi hao wakati wa ziara yake kutembelea ujenzi wa eneo la muda la Wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la viwanja vya Kibandamaiti Wilaya ya Mjini Unguja.
WANANCHI wa Mikunguni na Wafanyabiashara ya eneo la Kijangwani wakinyosha mkono kuomba kuwasilisha changamoto zao wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwa katika ziara yake kutembeleo eneo linalojengwa Soko la Wafanyabiashara wadogo katika eneo la Kibanda maiti Wilaya ya Mjini Unguja leo.
MWANANCHI wa Mikunguni Ndg.Mattar Salum  akiwasilisha changamoto za usafiri na kupatiwa nafasi  katika soko hilo  Vijana waliokuwa wakifanya kazi ya ulinzi katika eneo la kibanda maiti kabla ya kujengwa kwa soko la muda la Wafanyabishara ndogondogo, wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (haytupo pichani) wakati wa ziara yake kutembelea ujenzi wa Soko hilo
MFANYABISHA katika eneo la Kijangwani Bi. Maryam Abdalla akizungumza wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kutembelea eneo la Soko la muda kibanda maiti, linalotarajiwa kutumiwa na Wafanyabiashara kutoka eneo la kijangwaniu kuhamia katika eneo hilo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wananchi na Wafanyabishara wadogowadogo wanaotarajiwa kuhamishiwa katika eneo hilo baada ya kukamilika ujenzi wake ili kuweza kufanya biashara zao katika eneo hilo la Soko la Kibanda Maiti Wilaya ya Mjini Unguja akiwa katika ziara yake kutembelea ujenzi huo leo.6-3-2021 na (kushoto kwa Rais )Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana.
WAFANYABISHARA wa Kijangwani wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akizungumza na Wafanyabiashara hao katika viwanji vya Soko la Muda Kibanda maiti Wilaya ya Mjini akiwa katika ziara yake kujionea maendeleo ya ujenzi huo
WANANCHI wa enao la mikunguni na Wafanyabiashara wa eneo la Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wananchi hao wakati wa ziara yake kutembelea ujenzi wa eneo la muda la Wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la viwanja vya Kibandamaiti Wilaya ya Mjini Unguja leo 6-3-2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.