Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ahudhuria Hafla ya Kuapishwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu Chamwini Jijini Dodoma leo 31-3-2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mteule Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango.hafla hiyo imefanyika leo jioni 31-3-2021. wakiongozana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.Bashiri Ally. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya kuapishwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mteule Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango katika viwanja vya Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo.


Mhe. Philip Isdor Mpango akilia kiapo cha kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo 31-3-2021
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.Ibrahim Hamis Juma akimuapisha Mhe. Philip Isdor Mpango  kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo 31-3-2021
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.