Habari za Punde

Uzinduzi wa Mradi wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii,

KIJANA  Suleiman Said Humoud akitowa ushuhuda  yaliomkuta wakati akitumia dawa za kulevya na athari alizozipata wakati wa matumizi hayo na kupata msaada kupitia Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar( RAWWAZA) na sasa ameachana na matumizi ya Dawa za Kulevya, akitowa maelezo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimsikiliza mmoja wa shuhuda wa matumizi ya Dawa za Kulevya Ndg. Suleiman Said Humoud akitowa maelezo wakati wa uzinduzi wa Mradii wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, uliozinduliwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar na (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na (kulia kwake) Mwenyekiti wa Taasisi ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Mhe. Tauhida Cassian Gallos.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii wa Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) na Mshika Fedha wa Taasisi hiyo Bi, Valeria Rashid Haroub, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar tarehe 7-3-2021.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Risala ya Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) na Katibu wa Jumuiya hiyo Bi. Tatu Hussein Abdalla, wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar tarehe 7-3-2021.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Mhe. Tauhida Cassian Gallos, akizungumza na kutowa maelezo kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi kuzungumza na Wananchi na kuuzindua Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, hafla hiyo imefanyika katika ukumbiu wa hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar tarehe 7-3-2021.(Picha na Ikulu)

 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneze Kesho Yako, hafla hiyo imefanyika tarehe 7-3-2021, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.