Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Ziarani Kisiwani Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah akipokea kwenye Uwnja wa Ndege wa Pemba kuanza ziara ya Siku Tano kukaguwa miradi ya Maendeleo na kuona changamoto zinazowakabili Wananchi wa Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah akizungumza na Wakuu wa Taasisi Za Umma na zile zinazojitegemea Kisiwani Pemba katika Ukumbi wa Makonyo Wawi akianza ziara ya Siku Tano Kisiwani Pemba.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na.Othman Khamis OMPR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh.Hemed Suleiman Abdulla alisema Viongozi waliopata fursa ya kusimamia utumishi wa Umma wana dhima ya kuhakikisha wanawatumikia Wananchi wakati wote ili dhamira ya kuteuliwa kwao ileta mafanikio makubwa.

Alisema dhamana waliyokabidhiwa iliyozingatia vigezo na sifa walizonazo na kupelekea kuteuliwa kwao ni vyema zikatarajia kuleta ustawi kwa Umma uliowazunguuka mahali popote pale.

Mh. Hemed Suleiman Abdullah alisema hayo wakati akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Umma na zile za kujitegemea wakiongozw na Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote za Pemba hapo Ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Chake Chake akianza ziara ya ziku Tano Kisiwani humo kuangalia harakati za Maendeleo na changamoto zinazowakabili Wananchi.

Alisema zipo changamoto zinazowakabili Wananchi katika maeneo yao  ambazo kwa nafasi zao Wakuu hao wa Taasisi za Umma na zile za Kujitegemea wanalazimika kuzitafutia mbinu za ziada katika  kukabiliana nazo.

“ Zipo changamoto zisizohitaji gharama ya fedha lakini kinachoonekana kwa baadhi ya wakati ni uzembe ”. Alionya Makamu wa Pili wa Pili wa Rais wa Zanzuibar.

Mheshimiwa Hemed Suleiman aliwaeleza Wakuu hao wa Taasisi za Umma na zile zinazojitegemea kwamba bado wana nafasi nzuri ya kuishauri Serikali Kuu njia muwafaka ya mafanikio na kujiepusha na mifarakano pamoja na majungu yanayoviza Maendeleo.

Alibainisha wazi kwamba ni vyema wakathamini Kazi katika njia ya kuunganisha nguvu na mashirikiano kati ya Viongozi Wapya na wale Wakongwe na kuacha kasumba zinazoonekana kuendelea kufanywa na baadhi ya Watu waliokosa fursa kana hizo.

“ Yale matarajia ya Serikali kupitia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Hussein Ali Mwinyi ni vyema yakaanza kuonekana mapema”. Alisisitiza Mheshimiw Hemed Suleiman.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwatanabahisha Wakuu hao wa Taasisi za Umma na zile zinazojitegemea kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa ile ya Awamu ya Nane imedhamiria kuondosha uzembe, Rushwa na ubadhirifu wa Mali za Umma.

Alionya kwamba Kiongozi au Mtumishi ye yote atakayeshindwa kwenda na kasi ya Awani ya Nane ni vyema akaachia nafasi vyenginevyo Serikali haitakuwa na muhali wa kumuweka pembeni na kamwe haitazingatia nongwa za muhusika na baadhi ya Mitandao.

Alieleza kwamba yapo mafanikio makubwa yaliyoanza kuonekana na kuleta matumaini kutokana na Kasi ya Serikali inayokwenda sambamba na Ushirikiano wa Watumishi na Wananchi walio wengi katika maeneo mbali mbali ya huduma za Kijamii.

Mheshimiwa Hemed alisisitiza kwamba mafanikio yote yanayotarajiwa tayaendelea kupatikana kama Viongozi na Watendaji wote wataendelea kuzingatia umuhimu wa Maadili, Nidhamu pamoja na Heshima ya Uwajibikaji unaoambatana na Mshikamano.

“ Maadili ya Viongozi na Watumishi wa Umma lazima muda wote yakumbukwe katika muelekeo bora wa kutekeleza majukumu ya kila aliyepewa dhamana ya kuwatumikia Wananchi”. Alieleza Mh. Hemed Suleiman.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwatoa wasi wasi Wakuu wa Taasisi za Umma, Zile zinazojitegemea na Wananchi kwamba Serikali imeshajipanga kuona Malengo yake yanatekelezwa kwa mujibu wa Utaratibu uliowekwa akimaanisha zaidi masuala ya Uwekezaji.

Alibainisha wazi kwamba Kisiwa cha Pemba kitaimarika Kiuchumi kutokana na Mkakati madhubuti ya iliyowekwa na Serikali yakuwapa fursa nzuri Wawekezaji watakaojitokeza kuitumia nafasi hiyo maalum itakayosaidia kustawisha Umma hasa katika masuala ya Ajira.

Makamu Wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizipata meno Taasisi zinazosimamia ukusanyaji wa Mapato TRA na ZRB kuendelea kusimamia vyema jukumu lao na pale wanapoona uwepo wa ishara ya uvujaji wa mapato wasisite kutoa taarifa mara moja ili Taasisi zinazosimamia sheria zichukuwe hatua haraka.

Mheshimiwa Hemed alielezea matumaini yake kwa kubaini changamoto nyingi kupatiwa ufumbuzi ndani ya kipindi kifupi chini ya uratibu wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya maeneo ambayo Wananchi wanashauriwa kuendelea kuyatuimia ipasavyo.

Mapema Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mheshimiwa  Matar Zahor Masoud  kwa niaba ya Viongozi wa Mikoa Miwili ya Pemba, Wilaya zake Nne pamoja na Wananchi wake wanatoa Mkono wa pole kwa Viongozi wote wa Kitaifa kutokana na Msiba Mkubwa wa kufariki kwa Rais wa Awamu ya Tano Tanzania Marehemu Dr. John Pombe Magufuli.

Mheshimiwa Matar alisema huo ni msiba mzito uliyoikumba Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mnamo Tarehe 17 Machi wa kupoteza Kiongozi wake Mkuu akiwa bado madarakani.

Alisema Wananchi na Viongozi wote wa Kisiwa cha Pemba wataendelea kuungana na Watanzania wenzao mahali popote walipo katika maombolezo ya msiba huo wa siku 21.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.