Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Amejumuika na Wananchi Katika Sala ya Isha na Tarawekh Iliofanyika katika Masjid Sahar Kwarara.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Ibada ya Sala ya Tarawekh, ikiongozwa na Ust. Abdulsalam Juma iliyofanyika katika Masjid Sahar Kwarara  Wilaya ya Magharibi B Unguja, ikiwa ni muendelea wa Ibada ya Sala ya Tarawekh baada ya kumalizika kwa  Sala ya Isha katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume (kushoto kwa Rais) baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Tarawekh iliofanyika katika Masjid Sahar Kwarara Wilaya ya Magharibi B Unguja jana usiku 20-4-2021 na (kulia kwa Rais) Ust. Abdulsalam Juma
WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala ya Tarawekh, iliofanyika katika Masjid Sahar Kwarara Wilaya ya Magharibi  B Unguja, ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume.(hayupo pichani) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Waumini wa Dini ya Kiislam baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Tarawekh, iliofanyika katiuka Masjid Sahar Kwarara Wilaya ya Magharibi B Unguja jana usiku 20-4-2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wananchi wa Kwarara wakati akiondoka katika viwanja vya Masjid Sahar Kwarara Wilaya ya Magharibi B Unguja, baada ya kumalizika kwa Sala ya Tarawekh iliofanyika katika Masjid hiyo jana usiku 

BAADHI ya Watoto wakiwa katika viwanja vya Masjid Sahar Kwarara  baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Tarawekh wakimshangilia na kumsalimia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiondoka katika viwanja vya msikiti wa Masjid Sahar Kwarara jana usiku 20-4-2021
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.