Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza waandishi
wa habari hii leo katika Mji wa Serikali Mtumba kuelezea Kampeni kubwa ya
Mazingira na mashindano katika ngazi mbalimbali ikihusisha upandaji miti,
utunzaji na usafi wa mazingira itakayozinduliwa Siku ya Mazingira 5/6/2021 na Makamu
wa Rais Mhe. Philip Mpango.
Na Lulu Mussa. Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amesema Ofisi yake inaandaa Kampeni kubwa ya Mazingira itakayoenda sambamba na mashindano katika ngazi mbalimbali ikihusisha upandaji miti, utunzaji na usafi wa mazingira kwa ujumla wake.
Akizungumza wakati wa kikao
kazi na Menejimenti ya Ofisi yake pamoja na waandishi wa habari kilichofanyika
katika Mji wa Serikali Mtumba, Mhe. Jafo amesema kampeni hiyo kubwa na ya aina
yake itazinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Philip Mpango katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani tarehe 5 Juni
2021 kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa kielelezo katika utunzaji wa
mazingira.
“Kampeni hii kubwa
itahusisha Mikoa yote 26 na itahusu usafi na Utunzaji wa Mazingira kwa ujumla wake
ambapo tuzo na zawadi zitatolewa kwa washindi katika ngazi mbalimbali mara
baada ya tathmini kufanyika na zawadi zitatolewa wakati wa Siku ya Mazingira Duniani
Juni 5 mwaka 2021” Mhe. Jafo alisisitiza.
Kampeni hii pia
itashindanisha Majiji, Manispaa, Halmashauri za Miji na Majiji, Kata na Vijiji.
Katika nyanja za elimu na Afya, Vyuo, Shule za Sekondari, Shule za Msingi Hospitali,
Zahanati na Vituo vya afya pia zitashindanishwa.
“Tunafahamu changamoto kubwa
za usafiri katika mashule yetu na taasisi za elimu ya juu, zawadi kama Magari,
Pikipiki, Vifaa vya kufundishia na kompyuta zitatolewa, pia vifaa tiba katika
sekta ya afya ikiwemo vitanda katika hospitali zitakazoibuka vinara zitatolewa”
Jafo alisisitiza.
Makundi mengine yatakayoshindanishwa ni pamoja na Viwanda,
Migodi, Hifadhi za Taifa, Madampo, Viwanja vya Ndege, Stendi za Mabasi, Masoko,
Hoteli za nyota (1-5) na Waandishi wa Habari za Mazingira.
“Nataka kutoa rai kwa waandishi wa Habari wa magazeti, televisheni, bloggers na mitandaoni kushiriki katika kampeni hii na mashindano haya tuzo na zawadi zitatolewa kwenu” alisisitiza Mhe. Waziri
Aidha, ameiasa jamii na
watanzania kwa ujumla kupanda miti rafiki kwa mazingira hususan ile ya matunda kulingana
na jiografia ya maeneo yao kwa lengo la kuboresha na kuimarisha afya zao.
Katika kampeni hii kubwa na ya kipekee jumla ya washindi 152 kutoka makundi mbalimbali watapatikana na kupatiwa zawadi ikiwa ni pamoja na kupata fursa za kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo mbuga za Wanyama hapa nchini.
Sehemu ya Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani
Jafo (hayupo pichani) wakati wa kuelezea Kampeni kubwa ya Mazingira na
mashindano ya upandaji miti, utunzaji na usafi wa mazingira itakayozinduliwa
Siku ya Mazingira 5/6/2021 na Makamu wa Rais Mhe. Philip Mpango
Sehemu ya Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani
Jafo (hayupo pichani) wakati wa kuelezea Kampeni kubwa ya Mazingira na
mashindano ya upandaji miti, utunzaji na usafi wa mazingira itakayozinduliwa
Siku ya Mazingira 5/6/2021 na Makamu wa Rais Mhe. Philip Mpango.
Sehemu ya Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa kuelezea Kampeni kubwa ya Mazingira na mashindano ya upandaji miti, utunzaji na usafi wa mazingira itakayozinduliwa Siku ya Mazingira 5/6/2021 na Makamu wa Rais Mhe. Philip Mpango.
No comments:
Post a Comment