Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Ametengua Uteuzi wa Makamanda Watatu Vikosi Vya Idara Maalum za SMZ.Leo 12-4-2021.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa taarifa ya kuwepo kwa Wafanyakazi hewa katika Idara Maalum za SMZ, wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Makamanda watatu wa Idara Maalum za SMZ.

Waliotenguliwa ni Kamanda wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Ali Abdallah Ali, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kanali Ali Mtumweni Hamad na Mkuu wa Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) Comodore Hassan Mussa Mzee.

Akitoa taarifa maalum kwa wananchi kupitia vyombo vya Habari Ikulu Jijini Zanzibar, Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba kufuatia taarifa za uwepo wa wafanyakazi hewa katika Idara Maalum za SMZ, ambapo aliumda Kamati ya uchunguzi kwa kufanya uhakiki wa idadi ya wafanyakazi pamoja na viwango vya mishahara vinavyotolewa kwea vikosi vyote.

Akitoa taarifa kwa umma juu ya ripoti ya Kamati ya Uhakiki iliyomfikia kwamba kulikuwa na watumishi 381 waliokuwa wakilipwa mishahara bila ya kuwa katika utaratibu unaotakiwa ikiwa na maana kwamba hao ni watumishi hewa.

Alisema kwamba fedha zilikuwa zikipokelewa na kutumika katika kipindi chote hicho ambapo walikuwa katika vikosi hivyo na kueleza kwamba lililothibitika ni kwamba wakati Kamati imeanza kazi zake baadhi ya vikosi ikiwemo JKU walianza kutengeneza utaratibu wa kurasimisha uwepo wa wafanyakazi hewa.

Alsiema kwamba waliwahi kukamatwa baadhi ya Maafisa katika nyumba ya mtu binafsi wakiwa wawmewafisgha sare za Jeshi vijana na kuwapiga picha ili kuthibitisha kwamba wamo katika ajira rasmi.

Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba  imebainika kwamba fedha zilizotumika kwa upotevu ni kiasi cha TZS Bilioni mbili milioni mia mbili thalasini na tato laki saba na ishirini na tano kutokana na fedha zilizokuwa zikitumika kwawafanyakazi hao hewa.

Vile vile, Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba Kamati ilikwenda kuhakiki ulipaji wa posho katika vikosi hivyo ambapo ilibaini wastani wa upotevu wa fedha zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya posho kwa mwezi wa Disemba ni jumla ya TZS mia tatu na nne milioni laki moja thalathini na tano elfu mia tisa la thalathini na tisa.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.