Jeshi la Polisi limewataka
wananchi kutokuwa na hofu ya ulinzi na usalama wao siku ya uchaguzi Oktoba 29,
2025 na limewasihi wakapige kura na limewahakikishia kuwa hakutakuwa na
changamoto za kiusalama.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo leo Oktoba 24, 2025 mazungumzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu ya Polisi Kamisheni ya Zanzibar amesema Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na vikosi vyengine vya ulinzi na usalama limejipanga na limeweka
mikakati ya kuimarisha ulinzi wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Amesisitiza Jeshi la Polisi litawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria na halitakubali, halitamvumilia mtu au kikundi kitakachojaribu kuchochea ghasia, Kuhamasisha maandamano haramu au Kuwashawishi wananchi kuvunja sheria.
Kitengo cha Habari
Makao Makuu ya Polisi
Kamisheni ya Zanzibar.

No comments:
Post a Comment