Habari za Punde

Ziara ya Makamu wa Pili wa Rais Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla akitoa saa 24 kwa Soko la Mombasa Shimoni kurejea kwa Mnada uliosita kwenye soko hilo kwa takriban Mwaka Mmoja sasa akiwa katika ziara ya Wilaya ya Magharibi B kukagua shughuli za Maendeleo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla akiwatahadharisha Wahandisi na Washauri Elekezi wa Miradi ya Maendeleo kuwa makini na Wakandarasi wa ujenzi wasiozingatia Mikataba wakati alipokagua Mitaro ya Maji ya Mvua iliyojengwa chini ya Kiwango na kuleta athari kwa Makaazi ya Wananchi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla akiwa na Ujumbe wake akilikagua Bwawa la jangamizini na kushauri Kuundwa Kamati itakachunguza ongezek la Kina cha Maji katika Bwawa na hilo na kushauri hatua za kutekelezwa katika kipindi kifupi.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na.Othman Khamis.OMPR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameuagiza Uongozi wa Mkoa Mjini Magharibi kuurejesha mnada uliokuwepo katika Soko la Mombasa shimoni ambao umesimamishwa  kwa takriban Mwaka Mmoja sasa.

Akishangiriwa na Wafanyabiashara wa soko hilo kufuiatia kauli hiyo akiwa katika ziara ya Wilaya ya Magharibi B katika mfululizo wa ziara zake kuangalia maendeleo na chngamoto zilizomo  katika Wilaya zote Mh. Hemed alisema  Mkoa lazima utafakari Mnada kwenye Masoko yote  kwa kuzingatia mahitaji halisi.

Mh. Hemed alisema kuanzia saa 24 zijazo akimaanisha asubuhi ya Jumatano mnada ndani ya Soko hilo la Mombasa urejee kama kawaida ili kuwapa fursa Wananchi na hasa Wafanyabiashara  kupata huduma na riziki zao za halali.

Alifahamisha kwamba si vyema Mwananchi akalazimishwa kufuata bidhaa muhimu za vyakula katika masafa marefu  wakati uwezo wa kufuata huduma hizo katyika masoko ya karibu unawezekano endapo utapangwa utaratibu mzuri.

Mheshimiwa Hemed alkitoa indhari kwa Wafanyabiashara kuendelea kufuata Sheria na taratibu zilizowekwa  kwa vile Serikali muda wote inapenda Wananchi wake  ambao nao kwa upande wao wana wajibu wa kuongeza ushirikiano wao kwa Serikali.

Kuhusu Milango ya Biashara Mheshimkiwa Hemed alionya kwamba kitendo cha Mfanyabiashara kupewa Mkataba wa kukodishwa Milango ya Biashara na baadae kumkodisha Mfanyabiashara mwengine  ni kuikosesha mapato Serikali Kuu. Aliutaka Uongozi wa Baraza la Manispaa Magharibi B kuwajibika kwa kumpangisha Mlango yule Mfanyabiashara wa Pili.

Alieleza kwamba hatua hii inastahiki izingatie ile kodi ya ziada anayotoa mkodishwa mwengine inaingia katika mfuko Mkuu wa Serikali badala ya fedha hizo kuendelea kuingia mifukoni mwa wajanja na matapeli.

Mheshimiwa Hemed alifahamisha kwamba wapo baadhi ya Wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kujilimbikizia milango mingi ya Biashara inayojengwa na kutolewa na Swerikali na huamua kushirikiana na baadhi ya Watendaji wa Taasisi za Umma wasio waadilifu tabia ambayo inapaswa kuonodhwa kwa kuopatiwa dawa ya kudumu.

Aliwaeleza Wafanyabiashara hao wa Masoko ya Mombasa, Mwanakwerekwe na Jumbi kwa Serikali Kuu kupitia Mabaraza ya Manispaa inaangalia mbinu muwafaka ya kujenga Soko Kubwa na la Kisasa katika eneo la Wilaya ya Magharibi B kwa lengo lka kuwaondoshea msongamano Wafanyabiashara wa Masoko hayo.

Akizungumzia changamoto ya mafuriko ya Mvua za Masika zinazoathiri maeneo mengi ambayo ujenzi wa  Bara bara ilifanyika na kuathiri Makaazi ya Wananchi, Mh. Hemed amewatahadharisha Wahandisi na Washauri Elekezi  wanaosimamia Miradi kuwa na hadhari na baadhi ya Wakandarasi wenye tabia ya kuodnosha njiani kazi wanazopewa.

Mheshimiwa Hemed alisema maeneo mengin yaliyopita Miundombinu ya Bara  bara  yamekuwa na matatizo kadhaa yanayosababishwa na ukosefu wa Mitaro ya kupitishia Maji machafu hasa wakati wa Kipindi cha Mvua kubwa za Masika.

Amewakumbusha Viongozi wa Mikoa, Wilaya na wale wa Taasisi husika za Umma lazima wafanye ziara za mara kwa mara kwa Wananchi tayari wameshajenga matumaini makubwa  juu ya uwajibikaji unaotekelezwa na Serikali yao.

Akilitembelea eneo la Bwawa la Jiangamizini kwa Gizo la Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi linalojaa maji ya Mvua hasa wakati wa msimu wa Masika makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman alisema Serikali itaunda Kamati Maalum ya kufanya utafiti utakaobaini chanzo cha ongezeko la maji katika Bwawa la Jangamizini.

Alisema Kamati hiyo itakayoundwa na kutoa Ripoti yake ndani ya kipindi kifupi kijacho itahusisha Wataalamu wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa, Mamlaka ya Mazingira, Ardhi, na baadhi ya Watu wanaoifahamu Historia na mwenendo halisi wa Bwawa hilo.

Mapema akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za Serikali za Wilaya ya Magharibi B hapo Ukumbi wa Halmashauri Mtaa wa Mombasa Mkuu wa Wilaya hiyo Bibi Hamida Khamis Mussa alisema vitendo vya udhalilishaji vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku.

Bibi Hamida alisema ongezeko hilo linatokana na kasi ya Jamii kujitokeza kuripoti matukio ya Vitendo hivyo vya udhalilishaji ambapo matukio 150 tayari yameshafikishwa katyika Mamlaka husika ambayo ni polisi kwa hatua za kisheria.

Alieleza kwamba Uongozi wa Wilaya kupitia Maafisa wake wa Ustawi  wa Jamii imekuwa ikiendelea kutoa Elimu ya jinsi Jamii inavyowajibika kushiriki kikamilifu  katika mapambano dhidi ya udhalilishaji hasa vile vya Ubakaji na Utelekezaji wa Familia unaosababishwa na Wanandoa kutalikiana.

Akigusia Migogoro ya Ardhi Bibi Hamida Khamis Mussa alibainisha kwamba uuzaji wa Viwanja kiholela kwa Eka zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Kilimo nan a hata Mashamba yanayorithiwa katika Familia ndio tatizo kubwa  linaloleta miogoro hiyo.

Alisema malalamiko 105 ya Migogoro ya Ardhi hasa katika Jamii yameripotiwa na hadi sasa 67 imeshapatiwa Ufumbuzi wakati 38 ikiendelea na mchakato wa kutafutiwa suluhu kwa kutumia Elimu kwa Wananchi juu ya kufuata Sheria pamoja na matumizi sahihi ya Ardhi.

Katika ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia alibahatika kutembelea Jengo jipya linalopjengwa la Mamlaka ya Chakula na Dawa, shughuli mbali mbali za Vijana pamoja na Kituo cha Machinjio ya Nyama kiliopo Kisakasaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.