Habari za Punde

Mbio za Mwenge Wilaya ya Mjini Unguja.

Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka (kulia) akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Maghribi “B”  Hamida Mussa Khamis  (kushoto) katika Viwanja vya Jeshi (JWTZ) Migombani Mjini Zanzibar.

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar . 

Kiongozi wa Mwenge Luten Joseaphine Paul Mwambashi amewata vijana kuitumia Teknelojia ya Tehama  kwa usahihi  na uwajibikaji ili iwaletee faida  sio kwa matumizi mabaya ya kuyarejesha nyuma maendeleo ya Taifa .

 

Akifunga Kongamano la vijana  huko Ukumbi wa Rahaleo amesema endapo wataitumia teknelojia hiyo itaweza kuwaletea faida na kupata  maendelea chanya kwa Taifa  kutokana na kurahisisha upatikanaji wa elimu na malipo katika ukusanyaji wa mapato ya serikali  .

 

Amesema kumekuwa na wimbi kuwa la Vijana wanaojishughulisha na utumiaji wa  mtandao kinyume na taratibu kufanya utapeli wa fedha uchochezi udanganjifu,udhalilishaji wa kijinsia pamoja na kusababisha  malezi mabaya kwa watoto na vijana

 

Hivyo ametoa rai kwa vijana  kuhakikisha kwamba wanatumia kwa usahihi Teknelojia ya Tehama ili kujenga  taifa endelevu na kuweza kupata maendeleo kwa haraka . 

 

Akizungumzia suala zima la mapambano dhidi ya maambukizi ya ukimwi amewataka vijana hao  kuepukana na vishawishi  vinavyopelekea maambukizi ikiwemo  kuachana na tamaa  kwani ugonjwa upo katika jamii na inapelekea kupunguza nguvu kazi ya Taifa na kuwashajihisha vijana hao kupima afya zao .

 

Aidha amesema Mbio za Mwenge zinasisitiza hasa mapambano dhidi ya  matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana kwani bado ni tishio jambo ambalo linaathiri nguvu kazi .

 

Akifahamisha kuwa mbio hizo zinasisitiza  mapambano juu ya Ugonjwa wa Malaria ambao huwapata mama wajawazito na watoto hivyo Kiongozi huyo alitoa rai ya kufanya usafi wa mazingira yanayowuzunguka ili kuua mazalio ya mbu pamoja na kutumia vyandarua vilivyoweke dawa .

 

Hata hivyo wakati Kiongozi wa Mbio za mwenge akizindua mfumo wa kisasa wa teknolojia  Msoma  Risala Afisa Habari wa Wilaya ya Mjini, Msangu Said amesema katika tathnia hiyo kuna changamoto ya upungufu wa ujuzi kwa vitendo ukosefu wa sera na taratibu ya kuondoa mali ya tehama pamoja na kukosekana kwa wafanyakazi waliofunzwa tathnia hiyo .

 

alifahamisha kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt . Hussein Ali Mwinyi amekusudia kuijenga Zanzibar mpya kupitia uchumi wa kisasa

( Blue Economy) ambao una mpango mkakati wa kuendeleza wananchi na wafanyakazi kiujumla kuweka  ufanisi na kuengeza dhamani katika mfumo wa mazingira ya Tehama.

 

Kiongozi huyo aliweza kufungua miradi mbali mbali katika  Wilaya ya Mjini ikiwemo Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vijana wa Shehia ya Bintihamrani ,Mradi wa Maji Chumbuni, ufunguzi wa  Studio ya Stone Town  na Menginezo.

Kiongozi Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021  Luteni Josephine Mwambashi (kulia) akipata maelezo kuhusu bwawa la kufugia samaki kwa msimamizi wa mradi wa ufugaji samaki kutoka Baraza la vijana Shehia ya Bitihamrani Abdulhali  Khamisi  (katikati) wakati mbio za mwenge zilipokagua mradi huo huko kwa Biti Hamrani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka.
Mwakilishi wa Jimbo la  Mpendae Shaabani Ali Othmani akiahidi milioni saba kwa ajili ya kusaidia Mradi wa majaribio wa ufugaji samaki  Shehia ya Kwa Biti Hamrani .
Kiongozi Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Luteni Josephine Mwambashi (wapili kulia) akifungua bomba la maji safi na salama katika kisima kilichopo  JKU Chumbuni ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho huko Chumbuni Wilaya ya Mjini Zanzibar.
Kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Luteni Josephine Mwambashi akikabidhi vyeti kwa baadhi ya Vijana wa Wilaya ya Mjini waliyohitimu Mafunzo ya Tehama yaliyoandaliwa na Baraza la Vijana la  Wilaya hiyo mara baada ya kufunga mafunzo  huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.  
Kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Luteni Josephine Mwambashi akikabidhi vyeti kwa baadhi ya Vijana wa Wilaya ya Mjini waliyohitimu Mafunzo ya Tehama yaliyoandaliwa na Baraza la Vijana la  Wilaya hiyo mara baada ya kufunga mafunzo  huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.  
Wanafunzi wa Wilaya ya Mjini wakiimba wimbo maalum katika  zoezi la  Upimaji wa afya na uchangiaji damu mara walipopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru kukagua zoezi hilo huko Mapinduzi Squre Kisonge Wilaya ya Mjini Zanzibar.
Kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Luteni Josephine Mwambashi akikabidhi vyandarua kwa baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Mjini katika  zoezi la  Upimaji wa afya na uchangiaji damu huko Mnara wa Kumbukumbu Mapinduzi Squre Kisonge.
Kiongozi Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Luteni Josephine Mwambashi akikagua mfumo wa Tehama Ulioandaliwa na Wilaya Ya Mjini ambao utatoa taarifa zote za Wilaya ya Mjini huko Nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Vijana wenye mahitaji maalum wakiimba  wimbo  maalum katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Luteni josphin Mwambashi akionyesha zawadi maalum aliyopewa na Vijana wa Stone Town Records huko katika ukumbi  wa  Shekh  Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar. 
Kiongozi Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Luteni Josephine Mwambashi akikabidhi kigari kwa Mtoto mwenye mahitaji maalum katika Ukumbi wa  Shekh  Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Picha na Fauzia Mussa - Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.