Habari za Punde

Prof. Mkumbo Akipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa Kubuni Utaratibu wa Mashindano ya Ubunifu na Ujasiriamali

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akifungua fainali za Ubunifu na Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na siku ya wanafunzi ya Ubunifu na Ujasiriamali inayoadhimishwa kila mwaka  na iliyokuwa na kauli mbiu inayosema “Badili Changamoto kuwa Fursa”, Mei 08, 2021 katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Na Eliud Rwechungura

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kubuni utaratibu wa mashindano ya wanafunzi ya Ubunifu na Ujasiriamali inayofanyika kila mwaka.

Prof. Mkumbo ameyasema hayo Mei 08, 2021 katika siku ya wanafunzi ya Ubunifu na Ujasiriamali na fainali za Ubunifu na Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika ukumbi wa Nkrumah iliyokuwa na kauli mbiu inayosema “Badili Changamoto kuwa Fursa”

“Nakipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kubuni utaratibu kama huu wa kusaidia kuibua na kukuza vipaji vya ubunifu vya vijana wetu katika kujibu matatizo ya jamii. Mimi hapa ni nyumbani, hivyo najisikia vizuri kuwepo hapa na kushiriki pamoja nayi” ameeleza Prof. Kilila Mkumbo

Prof. Kitila ameeleza kuwa ujuzi unaotakiwa katika soko la ajira na nini wanafunzi wafundishwe ili wakubalike katika soko la ajira lina mjadala mrefu duniani kote.

Prof. Kitila amesisitiza kuwa tafiti zinaonesha kuwa mataifa yaliyoendelea kama Marekani na Ulaya yameingiza elimu ya ujasiriamali katika mitaala yao zaidi ya miaka kumi iliyopita na kuleta matokeo chanya katika kuongeza fursa za wahitimu kupata ajira, kujiajiri, kutoa michango katika usitawi wa jamii na kukuza  uchumi.

Aidha, Prof Mkumbo wamewahakikishia mojawapo ya vipaumbele vya muhimu kabisa katika Wizara anayoiongoza ni kufanya kazi kwa nguvu zote ili kuhakikisha kwamba haiwakatishi tamaa vijana wenye mawazo ya ubunifu.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akifungua fainali za Ubunifu na Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na siku ya wanafunzi ya Ubunifu na Ujasiriamali inayoadhimishwa kila mwaka  na iliyokuwa na kauli mbiu inayosema “Badili Changamoto kuwa Fursa”, Mei 08, 2021 katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof. William Anangise akitoa maelezo na taarifa fupi namna chuo kikuu kilivyotilia mkazo kwenye ubunifu na elimu ya ujasiriamali katika fainali za Ubunifu na Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na siku ya wanafunzi ya Ubunifu na Ujasiriamali, Mei 08, 2021 katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof. William Anangise Pamoja na wageni waalikwa wengine wakifuatilia kwa ukaribu fainali za Ubunifu na Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ”, Mei 08, 2021 katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Baadhi ya Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wageni waalikwa waliohudhulia katika fainali za Ubunifu na Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na siku ya wanafunzi ya Ubunifu na Ujasiriamali inayoadhimishwa kila mwaka, ”, Mei 08, 2021 katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akikagua bidhaa mbalimbali zilizozalishwa na wajasiriamali wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika fainali za Ubunifu na Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na siku ya wanafunzi ya Ubunifu na Ujasiriamali inayoadhimishwa kila mwaka, ”, Mei 08, 2021 katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Picha zote na Eliud Rwechungura.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.