Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Hassan Chande (wa pili kushoto) akiwa katika ziara yake kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 katika mgodi mdogo wa Sekenke One uliopo wilayani Iramba Mkoa wa Singida kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. Hamad Hassan Chande (mwenye Kaunda suti)
akimwagalia mmoja wa vijana wanaojishughulisha na uchimbaji mdogo wa dhahabu akichenjua madini hayo alipotembelea mgodi mdogo wa Sekenke
One uliopo wilayani Iramba Mkoa wa Singida kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka
2004.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. Hamad Hassan Chande (mwenye Kaunda suti)
akizungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mgodi mdogo wa Sekenke One
uliopo wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) Kanda ya Kati, Dkt. Franklin
Rwezumula akifafanua jambo wakati wa mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mgodi mdogo wa Sekenke
One uliopo wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Hamad Hassan Chande amewataka wachimbaji wadogo wa dhahabu
kutotumia magogo katika shughuli zao kwa kuwa ni chanzo cha ukataji wa miti.
Chande ametoa rai hiyowakati
akizungumza na wachimbaji wa mgodi mdogo wa Sekenke One uliopo wilayani Iramba
Mkoa wa Singida alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004katika shughuli za uchimbaji.
Alisema kuwa imebainika wachimbaji wengi hukata miti kwa
ajili ya kujengea mashimo lakini alitahadharisha vitendo hivyo huchangia kwa
kiwango kikubwa uharibifu wa mazingira.
Aliwashauri watumie njia mbalimbali zikiwemo kujengea kwa
zege mashimo hayo kwa kuwa ni salama zaidi na pia huepusha vitendo vya ukataji
miti na hivyo kuendelea kuhifadhi mazingira.
“Tumekuja hapa kutembelea mgodi wenu na tumeona harakati
za uzalishaji wa madini ya dhahabu lakini nitoe wito kwa wamilikiwa migodi
wenye leseni tuache kukata miti na kutumia katika mashimo tutumie zege na kwa
kufanya hivyo tutapunguza ukataji miti,” alisema Naibu Waziri huyo.
Pamoja na kuendelea na shughuli hizo ambazo huwaingizia
kipato alitoa wito kwa wachimbaji hao kushiriki katika uhifadhi wa mazingira
ikiwemo zoezi la upandaji miti na kuitunza.
Pia, Naibu Waziri huyo alisema ni vyema wakawa wanafukia
mashimo baada ya kumaliza uchimbaji kwani ni chanzo cha uharibifu wa mazingira
na pia yanaweza kusababisha ajali lakini.
Kwa upande wake Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati, Dkt. Franklin Rwezumula alisema
Serikali imekuja na mradi wa kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu.
Alisema mradi huo ambao umeanza kutekelezwa utaifikia migodi
midogo mbalimbali nchini ukiwemo wa Sekenke One na utakuwa na manufaa makubwa
kwani utawasaidia kujifunza namna ya kufanya shughuli zao pasipo kuharibu
mazingira.
Dkt. Rwezumula alisema kupitia migodi ya mfano
itakayojengwa katika baadhi ya maeneo nchini wachimbaji wadogo watajifunza
mbinu bora za uchenjuji wa dhahabu bila kuathiri mazingira.
Aliwataka wenye kuendesha shughuli za migodi kusajili
miradi yao katika Baraza hilo kwa mujibu wa utaratibu ili zitambuliwe na
kusajili hatua na kukaguliwa na kupewa cheti pamoja ushauri inapohitajika.
Pamoja na hayo aliwataka pia kuwa na utaratibu mzuri wa
kuhifadhi taka za kemikali zinaztotumika katika shughuli zao hususan katika
uchenjuaji badala ya kuziacha zikizagaa ovyo hali inayiweza kuhatarisha afya za
wananchi wanaouzunguka migodi hiyo.
Naye Aifsa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,
Joseph Kiwango alisema Serikali kupitia Ofisi hiyo pamoja NEMC imekuja na Mpango
kazi kwa ajili ya kupunguza matumizi ya Zebaki kwa wachimnaji wadogo.
Alisema miongoni mwa shughuli zitakazotekelezwa kupitia
Mpango kazi huo wa miaka mitano ni pamoja na kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo
katika migodi mbalimbali takriban 40.
Pia Kiwango aliendelea kusisitiza kuwa Serikali
haijakataza matumizi wala uibngizaji wa Zebaki bali waingizaji wanapaswa
kujisaili kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kjtambulika
badala ya kuingiza kinyemea.
Shughuli za uchimbaji wa madini ni miongoni mwa vyanzo
vikuu vya mapato ya Taifa ambapo inaelezwa kuwa hadi kufikia Mei 2021 zaidi ya
sh. bilioni 4 zilikusanywa katika mgodi mdogo wa Sekenke wilayani Iramba mkoani
Singida.
No comments:
Post a Comment