Na john Mapepele. Mtwara.
Mikoa ya Shinyanga na Pwani imeongoza
kwenye mchezo wa kuruka chini katika Mashindano ya Taaluma na Michezo kwa Shule
za Sekondari (UMISSETA) kwenye fainali zilizofanyika leo Juni 29, 2021 katika
uwanja A kwenye chuo cha walimu mjini Mtwara.
Msemaji wa UMISSETA 2021, John
Mapepele amesema Musa Yusufu kutoka Shinyanga ameibuka kuwa mshindi wa kwanza baada
ya kuruka umbali wa mita 6 na sentimita 71 akifuatiwa na Mpaji Gipson kutoka mkoa
wa kigoma aliyeruka umbali wa mita 6 na sentimita 35 wakati nafasi ya tatu
imechukuliwa na Alexander Jumanne kutoka Mkoa wa Geita aliyeruka umbali wa mita
6 na sentimita 34.
Kwa upande wa wasichana Joha Mbaraka kutoka Mkoa
wa Pwani ndiye Mshindi wa kwanza kwa kuruka mita 4 na sentimita 72 akifuatiwa na
Witness Ibrahim kutoka Geita aliyeruka umbali wa mita 4 na sentimita 67 ambapo nafasi
ya tatu ilichukuliwa na Diana Chacha kutoka Mara aliyeruka umbali wa mita 4 na
sentimita 54.
No comments:
Post a Comment