Mikoa ya Arusha na Manyara imeongoza
kwenye mchezo wa Riadha mita 1500 katika Mashindano ya Taaluma na Michezo kwa Shule
za Sekondari (UMISSETA) kwenye fainali zilizofanyika leo Juni 29, 2021 mjini Mtwara.
Msemaji wa UMISSETA 2021, John
Mapepele amesema kwa upande wa wavulana Daniel Patric kutoka Arusha ameibuka
mshindi wa kwanza baada ya kumaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa dakika 4:07:16
akifuatiwa na Paul Ndege kutoka mkoa wa Mara aliyetumia dakika 4:11:06 wakati nafasi
ya tatu imechukuliwa na Agustino Leonard kutoka Mkoa wa Manyara aliyemaliza
mbio hizo kwa dakika 4:12:44.
Kwa upande wa wasichana Leoma Awaki kutoka Manyara
ameibuka mshindi wa kwanza baada ya kumaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa
dakika 4:44:50 akifuatiwa na Esther Martin kutoka mkoa wa Pwani aliyetumia
dakika 4:46:80 wakati nafasi ya tatu imechukuliwa na Nyanzobe Mbahi kutoka Mkoa
wa Mara aliyemaliza mbio hizo kwa dakika 4:49:66.
Kwa upande wa wasichana mkoa wa Njombe umeibuka mshindi wa kwanza katika mbio za kupokezana vijiti mita 4x100 (relay) kwa kutumia dakika (0:55:66), wakifuatiwa na mkoa wa Mara (B 0:56:16), mkoa wa Tabora umeshika nafasi ya tatu (0:56:19), mkoa wa Pwani nafasi ya nne (0:57:10) mkoa wa Simiyu nafasi ya tano (0:57:20) na mkoa wa Dodoma umeshika mkia (0:57:51)
No comments:
Post a Comment