Habari za Punde

Manispaa jiji la Zanzibar latakiwa kuweka mkakati kuhakikisha kwamba jiji lipo safi

Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohammed Mussa akielezea lengo la kikao hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum.
Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohammed Mussa akielezea lengo la kikao hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum.

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usimamizi wa Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma akitoa maelezo juu ya hatua watazochukua ili kuhakikisha kudhibiti uharibifu wa mazingira.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum akizungumza na Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohammed Mussa aliyefatana na ujumbe wake katika kikao cha pamoja kilichojadili hali ya usafi wa Mazingira katika Jiji la Zanzibar  huko Ofisini kwake Migombani Mjini Zanzibar

Picha na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar

Na Maryam Kidiko Maelezo Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum amesema Wizara yake ipo tayari kukaa pamoja na Manispaa ya Jiji la Zanzibar ili kuhakikisha kwamba jiji hilo linadumisha usafi na kuhifadhi mazingira.

Waziri Saada aliyasema hayo huko Ofisini kwake Migombani Mjini Zanzibar katika kikao cha pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohammed Mussa  na ujumbe wake kwa lengo la kujadili suala zima la Mazingira.

Alisema amashirikiano ya pamoja yataweza kusaidia kutelekeza vyema majukumu na kufikia lengo lilikusudiuwa katika utendaji kazi . 

“Ushirikiano ni kitu muhimu sana hivyo ipo haja kubwa kila mmoja kutoa mashirikiano kwa kukaa pamoja na kujadili suala la mazingira na kufikia muafaka”, alieleza Waziri Saada.

Alifahamisha kuwa manispaa ya Jiji ndio kiuvutio kikubwa kwa utalii ni vyema kudumisha usafi na kutunza mazingira ili kuimarisha uchumi wa nchi.

Nae Mstahiki Meya Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohammed Mussa alisema kuwa lengo kubwa la kuonana na Waziri Saada ni kujadili suala la mazingira na kupanga mikakati ya kuiumarisha usafi katika Jiji hilo ili kuwa ni kivutio nchini.

Alisema kuwa kutunza mazingira ni kuuweka mji katika taswira nzuri na haiba ambao ni chachu ya maendeeleo  hivyo ni vyema kujenga mashirikio  ya moja ili kufikia marajio ya kuepukana na majanga mbalimbali.

Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma alisema watahakikisha  kwamba Mamlaka inaweka mikakati madhubuti  itakayosaidia  kudhibiti uharibifu wa mazingira .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.