Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini, Khamis Hamza Chilo akizungumza na wananchi wa Jimbo la Uzini (hawapo pichani) wakati wa kutoa msaada wa kitoweo kwa ajili ya Skukuu ya Eid Hajj, katika Kiwanja cha Mpira Skuli ya Uzini
Baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea msaada wa kitoweo kwa ajili ya Skukuu ya Eid Hajj kutoka kwa Viongozi wa Jimbo la Uzini wakishirikiana na Jumuiya Kurbanla kutoka Nchini Uturuki katika Kiwanja cha mpira Skuli ya Uzini
Mwananchi wa shehia ya uzini Ali Juma Said, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wananchi wenzake wa Jimbo la Uzini mara baada ya kupokea msaada wa kitoweo kutoka kwa Viongozi wao wa Jimbo Wakishirikiana na Jumuiya ya Kurbanla kutoka Nchini Uturuki, huko Kiwanja cha mpira Skuli ya Uzini.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Haji Shaaban Waziri, akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari kuhusu msaada wa kitoweo uliotolewa na viongozi wa Jimbo la Uzini kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kurbanla kutoka Uturuki, katika Kiwanja cha Mpira Skuli ya Uzini.
No comments:
Post a Comment