Habari za Punde

Mkonge Uzalishwe Kwa Tija Ili urudisha Hadhi ya Tanga.

Na Hamida Kamchalla, KOROGWE.

ILI kuleta mapinduzi ya kilimo cha zao la kimkakati la mkonge ni lazima kuzalisha mkonge unaokwenda sokoni hivyo unapaswa kuzalishwa kwa tija huku kukiwa na ongezeko la tani zinazozalishwa ili kuleta uchumi wa Taifa ikiwa ni pamoja na kuirudisha hadhi ya mkoa wa Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Adamu Malima alisema jambo la kilimo cha zao hilo linaanzia wilayani Korogwe kwa kuanza mkakati wa kupeleka fedha kwenye kila Chama cha Ushirika mkoani humo huku akibainisha kwamba Vyama hivyo vina dhamana hivyo mtendaji yoyote atakayefanya vibaya atatimuliwa.

"Jambo la mapinduzi ya kilimo cha zao la mkonge linaanzia hapa wilayani Korogwe, Vyama vya Ushirika vina dhamana kwahiyo wale watakaotusababishia kushindwa tutawatimua, ukiwa na Ofisa kilimo wako kwenye Ushirika akifanya vibaya tutamtimua" alisema mkuu huyo.

"Miaka hamsini iliyopita mkonge ulikuwa ukizalishwa takribani tani elfu ishirini za zaidi kwa mwaka lakini ulienda ukashuka na sasa hivi unazalishwa tani elfu saba, lazima tuzalishe mkonge unaoenda sokoni hivyo tuzalishe kwa tija, katika mfano tuliokosea ni kufananisha nyimbo za siasa na kilimo, mimi naamini kama tumekuja hapa kwa nia moja na tupo tayari basi Mwenyezi Mungu atatuongoza" alibainisha.

Malima aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa Bima ya Afya kwa maendeleo ya Vyama vya Ushirika uliowashirika wadau wa maendeleo wakiwemo Benki ya CRDB, Bodi ya Mkonge mkoa, Vyama vya Ushirika pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uliofanyika jana wilayani Korogwe.

Alieleza kwamba zao hilo la kimkakati ni jambo kubwa la Kitaifa na kiuchumi pia hivyo kila Chama cha Ushirika kinapaswa kwenda kujifanyia tathminj na kuorodhesha yale waliyonayo ndani ya chama cha mrejesho ufike kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Saad Kambona ili naye atafute fedha kwa ajili ya Vyama hivyo.

"Kuanzia leo tunaweka mkakati mkoa wa Tanga kuleta fedha kwenye kila Chama cha Ushirika, kwahiyo kila Chama kiende kikafanye tathmini kutambua walichonacho ili Bodi ya Mkonge ikifika mapema mwezi huu Kambona akute mmeshajipanga" aliongeza.

Aidha alisema wakulima wote wanafanya kilimo chao kwa kutegemeana na Mashirika ya fedha na suala la wanaushirika kuwa na bima ni jambo jema lakini isitokee mkulima anakata bima na familia yake na mwisho wa aiku akifuata huduma anaanza kusumbuliwa.

"Wakulima wa aina yoyote, wote watafanya kilimo chao kwa kushirikiana na Taasisi za fedha, ila habari ya kwamba mkulima ana bima halafu analetewa habari ya kubabaisha babaisha hakuna, nawahimiza wakulima wangu wote mjiunge na hii huduma ya bima ya afya" alisema.

Malima alisema benki ya CRDB imeanza kuleta manufaa ya mikopo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatoa huduma za bima kwa wakulima hao hivyo kuwa kuwaomba Mashirika na wadau wengine wa maendeleo kuja kuboresha ili kwa pamoja kuhamasisha wananchi wengine katika upatikanaji wa huduma.

"Leo tumeanza na CRDB, nawaomba na wengine waje, twendeni tukaboreshe huduma ili sisi tuwe wasemaji wenu hukk mbele, mtakapobpresha watu wote watajisikia kujiunga na bima" alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.