Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbogwe Mhe. Nicodemas Maganga wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya upatikanaji wa mawasiliano katika kata ya Mbogwe zilipo ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.
Naibu Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kulia)n
akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe. Mhandisi Charles Kabeho wakiwa ofisi
ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kukagua hali ya upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika
Kata ya Mbogwe hususani katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo
Na Faraja Mpina, MBOGWE
Serikali kupitia
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni
1,015,000,000 kufikisha huduma ya mawasiliano katika Wilaya ya Mbogwe iliyopo
Mkoani Geita kupitia zabuni zilizotangazwa na Mfuko huo Juni 30 mwaka huu
Hayo ameyazungumza
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati wa ziara yake ya
kukagua hali ya upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika Wilaya hiyo ambapo
alizungumza na uongozi wa Wilaya hiyo pamoja na wananchi na kuwahakikishia kuwa
Serikali itawafikishia huduma ya mawasiliano kupitia bajeti ya mwaka huu wa
fedha 2021/22
Mhandisi Kundo
amesema kuwa ndani ya Wilaya ya Mbogwe Minara mitano ya mawasiliano itajengwa na
watoa huduma kupitia zabuni zilizotangazwa na UCSAF ili wananchi wa Wilaya hiyo
waweze kupata huduma za mawasiliano kwa sababu mawasiliano yanasaidia kukuza
uchumi, kuimarisha ulinzi na usalama na husaidia katika mazingira ya dharura
Ameongeza kuwa miongoni
mwa maeneo yatakayofikishiwa huduma ya mawasiliano ni pamoja na kata ya Mbogwe ilipo
ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo na ndipo jengo la ofisi mpya za Mkuu wa
Wilaya linaendelea kujengwa lakini bado hakuna mawasiliano
Aidha Mhandisi Kundo amesema
kuwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ambalo ndio linasimamia Mkongo wa
Taifa wa Mawasiliano tayari limeshafikisha Mkongo kwenye Ofisi za Halmashauri hiyo, hivyo mnara
utakaojengwa katika kata ya Mbogwe utakuwa ni wa TTCL
Naye Mkuu wa Wilaya
ya Mbogwe Mhe. Mhandisi Charles Kabeho amesema kuwa maeneo mengi ya wilaya hiyo
yana changamoto ya mawasiliano aidha kuwa na mawasiliano hafifu au kukosa
kabisa mawasiliano hivyo ujenzi wa Minara mitano katika Wilaya hiyo itasaidia
kutatua changamoto hiyo
Kwa upande wa Mbunge
wa Mbogwe Mhe. Nicodemas Maganga amesema kuwa anaishukuru Serikali kupitia
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kusikia kilio cha wananchi wa
jimbo lake cha kuwapelekea huduma za mawasiliano kwa kupeleka ujenzi wa minara
mitano ya mawasiliano katika maeneo yenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo
Katika Wilaya ya
Mbogwe minara ya mawasiliano itajengwa katika vijiji vya Nyasato, Kasosobe,
Ilolangulu, Iponya na ilipo Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe kupitia
zabuni ya awamu ya sita ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
No comments:
Post a Comment