Habari za Punde

Ufungaji wa Mkutano wa Kampeni za CCM Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Konde Pemba.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimnadi mgombea wa Ubunge Jimbo la Konde kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Sheha Mpemba Faki wakati wa ufungaji wa mkutano wa kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Konde.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimnadi mgombea wa Ubunge Jimbo la Konde kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Sheha Mpemba Faki wakati wa ufungaji wa mkutano wa kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Konde.
Viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi wakiunga mkono hotuba ya Mjumbe wa Kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akifunga Kampeni za Jimbo la Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi wakiunga mkono hotuba ya Mjumbe wa Kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akifunga Kampeni za Jimbo la Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Na.Kassim Abdi.OMPR.

Mjumbe wa Kamati kuu ya halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Mwinyi imedhamiria kutatua changamoto  zinawakabili wananchi wake, wakiwemo wananchi wa jimbo la Konde.

Mjumbe huyo wa Kamati kuu ameleza hayo katika mkutano wa ufungaji wa kampeni wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Konde unaotarajiwa kufanyika Julai 18mwaka huu.

Alisema katika kutekeleza ilani ya CCM, serikali imejipanga kutatua changamoto mbali mbali ndani ya jimbo hilo ikiwemo changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na kuzikarabati bara bara za ndani kwa kiwango cha lami,zilizokuwemo ndani ya jimbo hilo.

“Ndugu zangu wa jimbo hili la konde serikali inayosimamiwa na chama cha mapinduzi imepanga kufanya mambo mazuri katika nchi hii ikiwemo katika jimbo la Konde Mpeni kura mgombea wetu huyu Sheha Mpemba awatumikieni” Alisema Mhe. Hemed

Aliwahakikishia wananchi wa jimbo la konde kuwa serikali inayosimamiwa na chama cha mapinduzi inadhamiria kuwaondoshea  kero kutokana na dhamira ya dhati ya serikali ilionayo kwa wananchi wake.

Alieleza Chama cha Mapinduzi tangu kimeanza kuzindua kampeni zake katika jimbo hilo imekuwa ikihimiza Amani Utulivu  na Umoja ambapo CCM inaamini kufanya hivyo ndio msingi wa kupatikana kwa maendeleo.

Akiomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo, mgombea wa nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi ndugu Sheha Mpemba Faki aliwataka wananchi wa Jimbo la Konde kubadilisha fikra na mtazamo ili waweze kujikomboa kwani kwa miaka kadhaa sasa watu waliowaamini kutoka vyama vyengine wameshindwa kuwaletea maendeleo.

Akigusia sekta ya elimu mgombea huyo aliwaahidi wananchi kwamba endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Konde atahakikisha anapunguza Zero kwa wanafunzi wa jimbo hilo la kupandisha kiwango cha ufaulu kwani yeye ni mdau mmoja wapo anaeguswa na maendeleo ya elimu.

Alisisitiza kwamba katika kampeni zake alifanikiwa kuwafikia takribani makundi yote yaliokuwemo ndani ya Jimbo hilo jambo linatoa sura nzuri ya mafanikio kutokana wengi wa wapiga kura aliowafikia wameonesha kuridhika nae pamoja na kumuunga mkono.

Nae, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kaskazini Pemba alimuhakikishia mjumbe huyo wa Kamati kuwa akiwa yeye ni mwenye dhamana ya Mkoa wa Kaskazini Pemba kichama atahakikisha jimbo hilo kupitia uchaguzi huo wa Mbunge linachukuliwa na Chama cha Mapinduzi.

Kufuatia Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Julai 18, Chama cha Mapinduzi kimevitaka vyengine vya upinzani vilivyosiamamisha wagombea kuwa wastarabu kwa kuyakubali matokeo ya uchaguzi mara baada ya kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.