Habari za Punde

Ushirikiano Katika Utendaji wa Kazi Sekta ya Elimu Nchini Kutasaidia Kufikia Malengo.

Na Maulid Yussuf WEMA  ZANZIBAR

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amesema kushirikiana katika utendaji wa kazi kutasaidia kufikia malengo katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.

Akizungumza wakati wa kikao cha mashirikiano baina ya watendaji wa wizara ya Elimu Zanzibar na wa Tanzania bara, katika ukumbi wa Taasisi ya Utalii ya Chuo Kikuu cha  Taifa cha Zanziba SUZA Maruhubi Mjini Unguja amesema kushirikiana ni njia pekee ya kuweza kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu kwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amewataka watendaji wa pande mbili hizo kuhakikisha katika majadiliano yao wanazungumza kwa kuweka mikakati ya kutatua matatizo mbali ya Muungano kupitia sekta hiyo ya Elimu ili kuleta faida katika pande mbili hizo.

Amesema sekta ya elimu ni sekta mama katika kuleta maendeleo katika kila Taifa hivyo kunahitaji mtazamo wa hali ya juu katika kuondoa changamoto zikiwemo vitabu, Walimu mahiri pamoja na mambo yote yanayohusu sekta ya elimu.

Akizungumzia kuhusu somo la dini kutokua na sifa ya kuongeza alama za ufaulu wa  kujiunga na Chuo, Mhe Simai amewataka kukakikisha wanajadiliana kwa kukiwekea mazingira rafiki kwa kuliingiza  somo hilo ili kuondoa utata uliojitokeza.

Aidha amewanasihi watendaji hao kushirikiana kwa kila namna hasa Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo ili kuhakikisha mafanikio ya elimu yanapatikana kwa pande zote mbili za muungano wa Tanzania.

Nae katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar bwana Ali Khamis Juma amesema.......

Kwa upande wake katibu Mkuu Wizara ya Elimu Tanzania bara Dkt. Leonard Akwilapo  amesema ameshukuru kuendelea kufanyika mikutano kama hiyo ya mashirikiano baina ya Wizara hizo mbili ambayo italeta mafanikio makubwa katika ukiaji wa Elimu nchini.

Akiwasilisha ripoti ya Mradi wa kuboresha  wa Elimu ya Juu katika mageuzi ya uchumi ( HEET)  Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Tanzania Dkt  Kenedy Hosea amesema mradi huo umeshirikisha Vyuo 19 vya Tanzania bara na Visiwani.

Amesema pamoja na malengo hayo pia utalenga katika kubadilisha mitaala yenye tija kwa kuzingatia soko la ajira ambapo umepangiwa bajeti ya dola milioni  425.

Kupitia mradi huo Naibu Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA anaeshughulikia taaluma Dkt Ali Makame Ussi amesema, SUZA imejipanga kujenga majengi makubwa ikiwemo skuli ya kilimo pamoja na maabara yake na maabara ya kufundishia Sayansi, maabara ya maaomo ya sayansi ya kufundishia nasuala ya komputer na ofisi za  wafanyakazi.

Katika kikao hicho cha mashirikiano kati ya  watendaji wa wizara hizo mbili kimefanyika chini ya Mwenyekiti Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Ali Khamis Juma,ambapo kikawaida   hufanyika kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.