Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla Ameendelea za Ziara Yake ya Kushtukiza Katika Kituo cha Damu Salama.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed akikagua taarifa katika Kompyuta maalum ya kuhifadhia taarifa za damu zinazowasilishwa katika kituo cha damu salama wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwaagiza watendaji wa kituo cha Damu salama kuwa makini katika kuzihifadhi damu hizo kutokana na tegemeo la kuokoa maisha ya wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwaagiza watendaji wa kituo cha Damu salama kuwa makini katika kuzihifadhi damu hizo kutokana na tegemeo la kuokoa maisha ya wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akiwasili katika kituo cha Damu salama Amani Sebleni kwa Wazee kwa ajili ya kujionea mazingira ya utendaji kazi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho.

Na Kassim Abdi, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka watendaji wa serikali kusimamia vyema dhamana walizokabidhiwa ili kuongeza ufanisi katika mazingira ya kazi.

Mhe. Hemed alitoa  agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha Damu salama kilichopo Sebleni Amani Kwa wazee.

Alileza kuwa, wapo watendaji wazembe wasiopenda kutekeleza majukumu katika sehemu zao za kazi jambo ambalo amesema serikali itachukua hatua kwa lengo la kuimarisha utendaji katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Alisema Kituo cha damu salama kina umuhimu mkubwa katika kuokoa maisha ya watuhivyo kuna kila sababu kwa watendaji wenye dhamana ya kusimamia kituo hicho kufanya kazi kwa uwadilifu na uwaminifu ili kufanikisha lengo lililokusdiwa.

Akikagua maabara maalum ya kuchunguza na kuhifadhia damu Makamu wa Pili wa Rais alimtaka msimamizi wa maabara hiyo kuwa makini katika kuhakikisha damu hizo zilizochangiwa kwa hiyari na wananchi zinahifadhiwa kwa umakini mkubwa.

Aidha, katika kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizowasilishwa na wafanyakazi Mhe. Hemed alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa Wiazra ya Afya Dk. Abdalla Suleiman kuzichukua changamoto hizo na kupitia uongozi wa Wizara ya Afya angalie namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.

Akizungumzia changamoto ya gari maalum ya shughuli za damu salama Makamu wa Pili wa Rais aliitaka Wizara ya Afya kutoa kipaumbele kwa kulifanyia mataengenezo gari hilo ili liendelee kutumiwa nawafanyakazi katika kazi zao za kila siku.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais hakuridhishwa na utaratibu wa kuzihifadhi taka katika kituo hicho huku akimuagiza Mkurugenzi Mkuu huyo kuwasilisha taarifa kamili juu ya kuharibika kwa kifaa maalum cha Kuchomea taka ili kuepuka kuzaga kwa taka katika maeneo yasiokuwa rasmi.

Akielezea changamoto zinazowakabili wafanyakazi katika kituo hicho Fundi Sanifu wa Damu salama Madina Abdalla Khamis alimuleza Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Sulein Abdulla kuwa, kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi ikwemo usafiri, mafriji na mafriza ya kuhifadhia damu pamoja na mashine ya kufulia.

Mapema asubuhi, Makamu wa Pili wa Rais alifika katika kitu cha Afya cha Kwa Mtipura kujionea hali ya huduma zinazotolewa kwa wananchi katika kituo hicho.

Akiwa Kituoni hapo Mhe. Hemed aliwagiza wasimamizi wa kituo hicho kuangalia namna bora ya kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia wakati wanaofika vituoni huku wakizingatia kuchukua tahadhari ya kuwakusanya watu wengi kwa muda mrefu kutokana na maradhi ya Covid-19 sambamba na kufanya ukarabati kwa maeneo ambayo hayapo vizuri.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.