Habari za Punde

Watendaji Wakuu Wizara ya Elimu Wametakiwa Kuzitambua na Kuzisimamia Sheria za Kazi.

Na Maulid Yussuf WEMA  Zanzibar

Watendaji Wakuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wametakiwa kuzitambua na kuzisimamia sheria za kazi na kutoa maamuzi yanayo faa kwa watendaji wao ili kusaidia kuwepo mahusiano mazuri baina yao na watendaji.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ndugu Omar Ali Omar wakati wa warsha fupi kwa watendaji wa Wizara hiyo, yenye lengo la kuwazindua viongozi kuhusiana na sheria na kanuni za kazi katika ukumbi wa Wizara hiyo mazizini Mjini Unguja.

Amesema ni vyema kuwa na bidii ya kazi, kuheshimu haki za Binadamu, kuhudumia watu kwa heshima, pamoja na kuwa wawazi katika utendaji, kwani  kutasaidia kuleta ufanisi na utendaji bora katika nafasi zao.

Aidha  Amewaasa Watendaji hao kutotoa tarifa za uongo kazini na hivyo mtendaji huyo atakuwa ameenda kinyume na maadili ya kazi pamoja na sheria za utumishi.

Amewataka kutokuwa na tabia ya kumbagua mtu kutoka na Dini yake au kabila pamoja na Kujijengea mazingira ya kumuheshimu mkubwa na mdogo katika maeneo ya kazi na hiyo itasaidia kuleta utawala bora katika kazi.

Nao Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo wakitoa michango yao wamesema kiongozi mzuri ni yule anaeoongoza kwa kutumia kugha nzuri kwa anaowaoongoza na kuahidi kutoa maamuzi yao katika kazi bila kuathiri haki za watu ili kuleta ufanisi mzuri katika kazi.


Wamesema watajitahidi kufanya kazi kwa mashirikiano na viongozi wenzao pamoja na kutumia lugha nzuri kwani kufanya hivyo kutaleta tija na kutasaidia kuleta maendeleo mazuri katika taasisi.

Akihairisha warsha  hiyo  katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bw Ali Khamis Juma amewataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanapo toa mamuzi yao wanaweka ubinadamu bila ya kukiuka sheria na kanuni zilizo wekwa katika utendaji wao.

Pia amewataka kiwa na tabia ya kutoa taaluma kama hiyo ya kukumbushana kwa watendaji wengine ili kusaidia kuleta ufanisi mzuri katika kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.