Mkufunzi wa Mafunzo ni Mwandishi mwandamizi Ali N. Sultani akitoa mada kwenye mafunzo ya siku ya siku mbili kwa Maafisa Habari na tehama wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na taasisi zilizo chini ya Ofisi hio kwenye ukumbi wa mkutano wa uliopo Migombani, mjini Zanzibar
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak amewataka Maafisa
Habari wa ofisi hio pamoja na taasisi zilizo chini yake kuwa wabunifu katika
utendaji wao wa kazi na kutekeleza majukumu yao ipasavyo
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya
siku ya siku mbili kwa Maafisa Habari na tehama wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais na taasisi zilizo chini ya Ofisi hio kwenye ukumbi wa mkutano wa uliopo
Migombani, mjini Zanzibar
Dkt Shajak amewakumbusha Maafisa Habari hao
kutumia ujuzi wao na kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi na kwa wakati kupitia
tovuti, televisheni, redio, magazeti, majarida, mitandao ya kijamii
“Mafunzo
haya yanayowalenga nyinyi Maafisa Habari Mawasiliano na Uhusiano muweze kufanya
kazi kwa weledi na pia kujitathmini utendaji wenu kwani nina imani baada ya
mafunzo haya kutakuwa na mabadiliko katika utendaji wenu wa kazi jambo ambalo
litawawezesha wananchi kufahamu majukumu ya Ofisi hii nini tunakifanya, kipi
tunakitekeleza na matarajio yetu
Aidha Dkt Shajak amewataka maafisa hao vinara
katika kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na OMKR wakielewa kuwa majukumu
mahsusi ni Kuratibu masuala ya Uendeshaji, Utumishi na Mipango ya Ofisi,
Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa masuala yote ya kisera, mipango ya Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Kusimamia masuala ya Mazingira, Kuratibu na
kusimamia masuala ya Ukimwi, Kuratibu masuala ya Udhibiti wa dawa za kulevya,
na Kuratibu masuala ya Watu Wenye Ulemavu ili wananchi wafahamu maendeleo
yanayofanywa na Serikali yao kupitia OMKR.
”Ili majukumu haya yatekelezwe basi zinazotekeleza
sio sera nzuri wala sheria nzuri bali ni utekelezaji wa zile sera na ile sheria
yenyewe na wale wanaotekeleza wanahitaji taarifa zao si tu kufika kwa walengwa
lakini pia kufika zile taarifa sahihi kwa walengwa na wapelekaji wa taarifa hizo ni nyinyi maafisa habari ”
Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi ndugu Juma
Ali Simai amesema maafisa habari hawapaswi kuwa nyuma kutokana na mabadiliko
yanayotokea hivyo ni muhimu kupata muda wa kukumbushana na kufahamu mabadiliko
ya ulimwengu ili kwenda sambamba na fani yao
Nae Afisa Habari Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Raya Hamad Suleiman kwa niaba ya Maafisa Habari wameahidi
kutekeleza vyema majukumu yao kwa kuihabarisha jamii na kutoa ushauri kwani wao
ni daraja kati ya Ofisi hio Serikali na wananchi
Mkufunzi wa Mafunzo hayo ni Mwandishi
mwandamizi Ali N. Sultani, muongozaji na mtayarishaji wa vipindi ndugu Kassim
Kh. Jape na Mkuu wa Chuo cha Habari SUZA Bi Imane O. Duwe
Jumla ya mada tano zimeandaliwa katika mafunzo hayo ya siku mbili zikiwemo Umuhimu wa kuwa Afisa Habari, kazi na majukumu ya Afisa Habari, Uandaaji wa Documentari, Kuhariri video na uandishi wa skript, Jinsi ya kuandaa taarifa kwa waandishi na mkutano na waandishi wa habari pamoja na Matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari kupitia mitandao ya kijamii
No comments:
Post a Comment