Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Mpango Amekutana na Kuzungumza na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. wakati akiwasili katika ukumbi wa Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, hii leo Septemba 15,2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.