Habari za Punde

Mzee Sadalla Juma Sadalla (74) Aliyembaka mfanyakazi wake wa nyumbani Unguja, arudishwa rumande

Na Mwandishi wetu

Mshitakiwa Bwana Sadalla Juma Sadalla mwenye umri wa miaka 74 mkazi wa Bububu,Unguja aliyembaka  mfanyakazi wake wa ndani - house Girl wake mwenye umri wa miaka 15 amefikishwa Mahakamani  tena tarehe 14 Septemba 2021 katika Mahakama ya Vuga, Wilaya ya Mjini Unguja.

Baada ya kusimamishwa kizimbani Hakimu anayeendesha kesi yake ameamuru mshitakiwa arudishwe mahabusu hadi tarehe 29 Septemba 2021 wakati kesi hiyo itakaposikilizwa tena.

Mshitakiwa Bwana Sadalla Juma Sadalla anashitakiwa kwa kumbaka msichana wake wa kazi (jina linahifadhiwa)  na analalamikiwa na kuwa ni mzoefu wa tabia za ubakaji na mara nyingi kesi zake huzimaliza kienyeji lakini mara hii vyombo vya dola katika kukemesha vitendo vya ubakaji vimemtia nguvuni na kumfikisha  mbele ya sheria mahakamani.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inajitahidi kukomesha kabisa vitendo vya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia ambavyo vimeonekana kushamiri katika siku za karibuni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.