Habari za Punde

Watoto 113 Wakamatwa Kwa Tuhuma za Uhalifu.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Acp Safia Jongo akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali (hawapo pichani) wakati akitowa taarifa kwa waandishi wa habari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Acp Safia Jongo akionesha baadhi ya maguni 19 ya bangi yaliokamatwa yakiwa katika Kituo cha Polisi Tabora.

Na Lucas Raphael,Tabora

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia  watoto 113 kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu katika wilaya ya Nzega na Manispaa ya Tabora katika kipindi cha kuanzia Agasti na Septemba mwaka huu

Watoto hao waliokuwa wakijiusisha na matukio ya Wizi ,Uvunjaji na Ukataji wa mapanga huku watoto hao wakiwa na umri wa miaka 8 hadi 15 .

Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa polisi mkoani Tabora Acp Safia Jongo alisema kwamba kukamatwa kwa watoto hao kunafuatia msako unaoendelea mkoani hapa kukamata wahalifu mbalimbali kwa kipindi cha mwezi moja.

Alisema kwamba watoto haowalikuwa wakitumia  majina kwa ajili ya vikundi vyao ambapo wale wa Tabora manispaa walikuwa wanatumia jina la Nunda na wale wa wilaya ya Nzega walitumia majina ya Roho saba na Roho mbili.

Kamanda huyo wa polisi mkoani tabora aliendelea kusema kwamba watoto wa manispaa ya Tabora walikuwa wanafanya vitendo vya uhalifu kwa kuwajeruhi watu kupora kwa kushirikia na watu wazima ambao wamekuwa wakiwatuma kufanya uhalifu huo.

Alisema kwamba watoto wa wilaya ya nzega walikuwa wakivamia nyumba ambazo zinasubiria kuwekewa umeme kuingia na kuharibu miundombinu yake na kisha kuchukua nyanya nyekundu na kwenda kuuza kwa ajili ya kupata fedha.

Alisema matukio hayo yalisababisha watu wengi kupata hasara kwa kuharibiwa nyumba zao kitu ambacho wazazi wanapaswa kuwangali watoto wao kipindi cha usiku.

Alisema kwamba katika manispaa ya Tabora walikamatwa watoto 96 na Nzega watoto 17 jambo ambalo ni hatari sana kwa wazazi kushindwa kuwalea watoto wao.

Kamanda Safia  alisema baadhi yao wamefikishwa mahakamani ili mkono wa sheria uweze kufanya kazi yake na ikiwezekana ukomesha kabisa uhalifu mkoani hapa.

Hata hivyo aliataka wazazi kuangalia vyema watoto wao kwani wakiashwa bila kuchukuliwa sheria watakuwa wahalifu wabaya sana hapo baadaye.

Hata hivyo niwajibu wakila mzazi na mlezi kumlea vyema mtoto wake kwa kufuata maadili ya kitanzania ili kukomesha kabisa uhalifu”alisema Safia Jongo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.