Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt
Omar.D Shajak amelishukuru shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi
ya watu duniani UNFPA kwa juhudi inazozichukuwa katika kusaidia Watu wenye
Ulemavu
Ameeleza hayo
ofisini kwake Migombani alipofanya mazungumzo na Msaidizi Mwakilishi mkaazi wa
UNFPA Dkt Wilfred Ochan kuhusiana na nafasi ya Watu wenye Ulemavu katika
maendeleo ya nchi na kutoa shukurani kwa shirika hilo kwa kusaidia kuanzisha
mfumo jumuishi wa Watu wenye Ulemavu
Dkt Shajak amesema kuwepo kwa mfumo jumuishi wa Watu
wenye Ulemavu umekuwa ni suluhisho katika kuisaidia Serikali kufanya maamuzi
sahihi kwa vile unawezesha kujua idadi ya Watu wenye Ulemavu, aina ya ulemavu
wao na kiwango chake pamoja na mahitaji yao
Amesema mfumo jumuishi unaweka takwimu sahihi kufahamu
ukubwa na udogo wa mahitaji ya Watu wenye Ulemavu na hatimae serikali kufanya maamuzi
mazuri katika ya utekelezaji wa mipango yake kuanzia ngazi ya shehia hadi
serikali kuu
Aidha amesema pamoja na kuwepo kwa mfumo huo lakini
bado unahitaji maboresho ili uweze kwenda mbali hivyo kupitia UNFPA anaimani
wataweza kufikia malengo na watu wenye Ulemavu kupata stahiki zao zote ikiwemo
kuwajengea uwezo kielimu, afya na ushiriki wao katika masuala ya maendeleo ya
kiuchumi
Nae Msaidizi Mwakilishi mkaazi wa UNFPA Dkt Wilfred
Ochan amesifu jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa juhudi wanazozichukuwa katika
kuwasaidia Watu Wenye Ulemavu
Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha masuala ya Watu
wenye Ulemavu yanaendelea kutambuliwa na kuingizwa katika sera kwenye sekta
mbali mbali kama vile afya, elimu, miundombinu shirikishi, makaazi na ajira
ilikuwepo na ufanisi
Kupitia UNFPA wameahidi kuendelea kufanya kazi na
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la Watu wenye Ulemavu na kuona
namna ya kufanya mashauriano katika mpango mkuu wa miaka mitano ujao ili kuyaingiza
masuala ya Watu wenye Ulemavu yakiwemo masuala ya afya ya uzazi na kuwajengea
uwezo kielimu .
No comments:
Post a Comment