Habari za Punde

Walimu Wajengewe Uwezo Kupambana na Teknolojia ya Kasi ya Mabadiliko ya Dunia.Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akizungumza wakati wa kulifungua Kongamano la Walimu Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. na (kushoto kwake) Wazri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said. 
Walimu kutoka Skuli mbalimbali wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Kongamano la Walimu ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani inayotarajiwa kufanyika Oktoba 5, 2021, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba ni muhimu kwa walimu kujengewa uwezo zaidi ili kuwa sambamba na mahitaji ya elimu yanayokwenda na kasi ya mabadiliko ya dunia.

Mhe. Makamu ameyasema hayo leo, alipofungua kongamano la walimu huko katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni mjini Zanzibar, ikiwa ni matayarisho ya kuelekea kilele cha Siku ya Walimu Duniani inayoadhimishwa tarehe 5 Oktoba, ya kila mwaka.

Amefahamisha kwamba, hivi sasa elimu imetanuka sana kutokana na kuwepo kasi kubwa ya mabadiliko na maendeleo ya sayansi na Teknolojia na kwamba katika mazingira hayo ni vyema kuwepo mikakati madhubuti itakayosaidia kujenga mfumo bora na imara wa kuwaongeza uwezo wa walimu hapa nchini.

Akizungumzia hadhi ya walimu hapa Zanzibar, Mhe. Othman amesema imeshuka na kuitaka jamii na hasa walimu kuweka mikakati ya suluhisho la vikwazo katika maendeleo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.