Habari za Punde

Zantel yazindua huduma ya Lipa kwa Simu, njia rahisi zaidi ya kufanya malipo kidigitali

 

Viongozi mbalimbali wa Kampuni ya Zantel wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa huduma ya Lipa Kwa Simu uliofanyika katika soko la Darajani mjini Unguja.Huduma ya Lipa kwa Simu inawasaidia wateja kulipia bidhaa na huduma kwa simu kupitia QR Code au Menyu

Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa akizungumza na wanahabari kuhusu huduma ya Lipa Kwa Simu inayowawezesha wateja kulipia huduma na bidhaa kidigitali.Kulia ni Mkuu wa Idara ya Malipo Salum Mohammed Nassor.

Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa akizungumza na mfanyabiashara Ali Ramadhan Mzee kuhusu huduma ya LIPA KWA SIMU ambayo inawasaidia wafanyabiashara kupokea malipo kwa urahisi kwa njia ya simu kutoka mitandao yote.Katikati ni Afisa wa Ezypesa Eunice Alelyo.


Unguja. November Mosi,2021. Bila kujali mtandao wa simu uliopo, sasa unaweza kulipia huduma na bidhaa kwa wafanyabiashara zaidi ya 800 hapa Zanzibar kupitia huduma ya Lipa kwa Simu.

Huduma hii imeboreshwa ambapo kwa mara ya kwanza ilijulikana kama Lipa Hapa iliyozinduliwa mwaka 2019. Lipa kwa Simu inakuja na sifa muhimu ikiwamo mfumo wa QR Code ambayo ni rahisi zaidi kutumia.

Kupitia Lipa kwa Simu wafanyabiashara mbalimbali na taasisi zitaweza kupokea malipo kwa njia ya simu kutoka kwa wateja wa mitandao yote.Ni huduma ya uhakika na salama kwa wafanyabiashara na wateja.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa alisema “Tupo kwenye ulimwengu wa kidigitali ambao unatoa fursa nyingi hasa kwenye teknolojia za malipo.Kama kampuni ya kibunifu tumetumia fursa hizo ili kuongeza ubora wa huduma kwa wateja wetu,’ alisema.

“Tunaamini kuwa, huduma hii ya Lipa Kwa Simu, itawapa wateja wa Ezypesa na wale wa mitandao mingine uhuru wa kufanya malipo kwa usalama, haraka na mahali popote kwa wafanyabiashara wa aina zote,” alisema.

Alisema kuanzishwa kwa mfumo wa QR Code kwenye huduma hiyo unatarajia kuongeza ufanisi na urahisi wa kufanya malipo tofauti na ilikuwa awali.

“Ili kutumia mfumo huu, mteja atatakiwa kupakua App ya Ezypesa na kisha kuscan kwenye QR Code ambazo zinapatikana kwa wafanyabiashara wote waliosajiliwa.Kwa wale ambao hawana simu janja watatumia menyu ya Ezypesa *150*02# au menyu ya mtandao mwingine,” alisema

Kwa wafanyabiashara, huduma hii ni muafaka kwao kwani itawasaidia kuondoa kero mbalimbali na kuwapa muda wa kusimamia shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Moja ya faida ni kutosumbuka kutafuta chenchi kwani wateja watalipia moja kwa moja kwa njia ya simu.Pia, usalama wa pes ani mkubwa zaidi kwani pesa za mauzo zitahifadhiwa kwenye akaunti ya Ezypesa ambapo zitaweza kuhamishika kwenda benki, kutuma kwenda kwa mfanyabiashara mwingine au kufanya malipo.

Wateja wanaweza kufanya malipo kwenye maeneo kama vile masoko, vitu vya mafuta, migahawa, hoteli, baa, maduka ya dawa, maduka ya vifaa vya ujenzi na mengineyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.