Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar ( PBZ ) Yakabidhi Zawadi Shilingi 1,000,000/= Kwa Wanafunzi wa Kidatu cha Sita Waliopata Division One Zanzibar.

Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar Ndg.Iddi Khamis Haji (kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PBZ Dkt.Estella Ng'oma Hassan na Mkurugenzi Muendeshaji wa PBZ Dkt.Muhsin Salim Masoud, wakimkabidhi zawadi Mwanafunzi wa Kidatu cha Sita aliyefanya vizuri mitihani yake ya Kidatu cha Sita na kupata Division One  Nasra Ali Seif, hafla hiyo ya kukabidhi zawadi iliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Bima Mpirani Jijini Zanzibar leo 12-12-2021.

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ BANK), leo imetowa zawadi ya Tsh. 1,000,000/= kwa kila Mwanafunzi aliyepata Daraja la Kwanza (DIVISION ONE) SAYANSI, Kidato cha Sita 2019/2020, Zanzibar. Shuhuli  hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shirika la Bima la Zanzibar, Mpirani chini ya Ugeni Rasmi wa Ndugu. Idd Khamis Haji, Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar.

Pia kwakutambuwa umuhimu wa masuala ya kielimu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PBZ, Dr Estella Ng'oma Hassan na Mkurugenzi Mwendeshaji wa PBZ, wamehudhuria shuhuli hiyo ambapo wamepata fursa ya kutowa nasaha zao kwa wanafunzi hao.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar Ndg.Iddi Khamis Haji (kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PBZ Dkt.Estella Ng'oma Hassan na Mkurugenzi Muendeshaji wa PBZ Dkt.Muhsin Salim Masoud, wakimkabidhi zawadi Mwanafunzi wa Kidatu cha Sita aliyefanya vizuri mitihani yake ya Kidatu cha Sita na kupata Division One  Abdallah Omar Mohammed, hafla hiyo ya kukabidhi zawadi iliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Bima Mpirani Jijini Zanzibar leo 12-12-2021.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar Ndg.Iddi Khamis Haji (kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PBZ Dkt.Estella Ng'oma Hassan na Mkurugenzi Muendeshaji wa PBZ Dkt.Muhsin Salim Masoud, wakimkabidhi Mama Mzazi wa Mwanafunzi Kidatu cha Sita aliyepata Division One Abdulrahaman Zaidu Mohammed, Mama Rukia Asad Mussa, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi iliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Bima Mpirani Jijini Zanzibar leo 12-12-2021.
Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Dkt.Muhsin Salim Masoud akizungumza wakati wa hafla ya kuwazawadi Wanafunzi wa Kidatu cha Sita Zanzibar waliofanyika vizuri masomo yao ya Sayansi katika Mtihani wa Kidatu cha Sita na kufaulu kwa daraja la Kwanza (Division One) hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Bima Mpirani Jijini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PBZ Dkt.Estella Ng'oma Hassan akizungumza na kuwapongeza Wanafunzi wa Kidatu cha Sita Zanzibar waliofanya vizuri na kushika nafasi ya  Daraja la Kwanza (Division One) masomo ya Sayansi, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya fedha shilingi Milioni Moja kila Mwanafunzi aliyepata Division One, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Bima Mpirani Jijini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar Ndg.Iddi Khamis Haji akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi iliyotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa Wanafunzi wa Kidatu cha Sita waliopata Division One Somo la Sayansi Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Bima Mpirani Jijini Zanzibar na (kulia ) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PBZ Dkt.Estella Ng'oma Hassan na (kushoto) Mkurugenzi Muendeshaji wa PBZ Dkt.Muhsin Salim Masoud.




 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.