Habari za Punde

Droo ya Upangaji wa Makundi ya Timu na Ratiba Mashindano ya Taifa CUP 202.

 

.  Shafi Dauda (kushoto) na Baraka Kizuguzo ambaye ni Afisa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) wakichezesha  droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba  ya mashindano ya Taifa CUP 2021.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul akishuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar es Salaam. Kushoto Kaimu Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa. Bi Neema Msita, kulia Mkurugenzi wa Michezo. Yusuf Omary Singo.


Na John Mapepele.                                                                    

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul leo, Disemba 7, 2021 ameshuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika tukio hilo amesema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kurejesha mashindano hayo ambayo yalikuwa yamesimama kwa miaka kadhaa.

Aidha amesema mashindano ya mwaka huu yameboreshwa   tofauti na yale ya awali.

Amesema maboresho hayo ni pamoja na kuingiza michezo mitatu; soka kwa wanaume na wanawake, netiboli na riadha kwa wanaume na wanawake ambapo awali ulikuwa mchezo mmoja tu wa soka.

Pia amesema mashindano haya yameshirikisha pande zote mbili za Tanzania ili kuwa na sura ya kitaifa

Ametoa rai kwa vyama vya michezo na mashirikisho kuja kwenye mashindano hayo ili kuona vipaji vya wachezaji ambao wanaweza kuwachukua kwenye vilabu vyao.

Akizungumzia dhana ya Taifa CUP amesema  lengo la mashindano hayo ni  kuwashirikisha wanamichezo  kutoka mikoa yote nchini ambapo  amesisitiza kuwa  mashindano hayo yanasaidia  kuleta umoja na mshikamano, kutoa ajira na kuimarisha afya za wachezaji hao.

Akimkaribisha Mhe. Gekul  kutoa hotuba fupi kabla ya kuchezesha droo hiyo Mkurugenzi wa Michezo nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandlizi ya Taifa CUP, Yusufu Omary Singo amesema  droo hiyo imechezeshwa  kwa uwazi ili kuyafanya yawe wazi zaidi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.