Habari za Punde

Kaka Mkuu Huwa Hafukuzwi Shule.

 
Na.Adeladius Makwega -Dodoma

Neno Kiranja lina maana kadhaa ikiwamo la kiongozi wa vijana wanaopelekwa jandoni pamoja na mara zote kiranja huwa wakwanza kutahiriwa siku hiyo ya jando ni ndiyo maana hukabidhiwa majukumu kama mkuu wa kundi nzima jandoni.Yapo maneno mengine ya kiswahili yenye maana hiyo ambayo ni Fumbi na Chando.

Kwa utaratibu wa jando ulivyo ngariba mara nyingi huwa ni mtu ambaye anakodishwa kwenda kuifanya kazi hiyo kwa hiyo wakaazi husika hujipanga na kuhakikisha wanakuwa na mahitaji yote yanayohitaji kwa kazi hiyo ikiwamo na namna watakavyomlipa ngariba(fundi) maanadalizi yakishafanyika basi hapo ndipo mjumbe hutumwa hadi kwa ngariba na kumwambia kuwa sasa kazi kule imekamilika na malipo yako yapo tayaria na zoezi letu litawahusisha vijana kadhaa. Hapo ngariba hufika kuhitimisha zoezi hilo.

Baada ya ngariba kufika ataifanya kazi yake vizuri na kusimimia zoezi hilo hadi vidonda vya vijana wake viwe vimepona na kuhakikisha kila kijana zoezi hilo linalofanyika limefanyika vizuri na kwa uhodari na hapo tamati ndipo vijana hao watakabidhiwa kwa wazazi wao. Hapo sasa lazima panakuwa na sherehe kubwa huku ukiliwa wali na kuchinjwa kwa wanyama kama vile mbuzi na ng’ombe. Kuchinjwa kwa wanyama hao kunaweza kufanyika kwa shirika au kwa binafsi binafsi kila mmoja akachinja wake katika makaazi ya familia mara baada ya vijana hao kutoka jandoni.

Vijana hawa wakiwa jandoni hufunzwa mengi sana lakini mojawapo kubwa ni kuhakikisha wanaheshimiana sana miongoni mwa wao kwa wao lakini heshimu ilipewa msisitizo kumuheshimu kaka yao mkubwa yule aliyefungua dimba wakati wa zoezi hilo linafanywa na ngariba. Huyu sasa ndiye kiranja.Kitendo cha kumvunjia heshima Kiranja hukumu yake ilikuwa ni kurudisha tena jandoni ambapo sasa uliingizwa na watoto wadogo na umri wako. Huku ikitamkwa kuwa utatahiriwa tena lakini hoja ya huko ilikuwa ni ya kuyarudia mafunzo ili kupata elimu ya kina juu ya kuheshimu waliokutangulia.

Kitendo cha kuambiwa unarudishwa tena jandoni kilikuwa ni aibu ya mwaka kwa anayefanyiwa hivyo na, familia yake na ukoo wake wakitambulika kuwa wao ni binadamu wasiokamilika kwa hiyo hilo lilikuwa ni jambo la nadra sana kutokea lakini lilipotokea kulikuwa hakuna budi. Wakati mafunzo haya yakiendelea mhusika huyo aliyerudishwa mara ya pili huko hupatiwa mikwaju ya maana.

Kiranja akiwa jandoni huwa anashirikishwa na mambo kadhaa na ngariba  pamoja na watu wazima kadhaa ambao wapo pamoja na vijana hao msituni kuhakikisha kwa imani yao pengine watu wabaya wasiwafikie hapo walipo maana watu wabaya wanaweza kuwaombea mbaya na vidonda vikachelewa kupona na mwisho vijana wakapata madhara.

Tulipoanzisha utaratibu wa shule nasi tulipokuwa tunamtafuta kiongozi wa wanafunzi tulimuita kiranja huku kiranja/kaka Mkuu/ Dada Mkuu yote yakimanisha kuwa ni kiongozi wa vijana  katika shule . ambaye anajukumu la kuwasimia wanafunzi wenzake katika mazingira ya shuleni na wakati mwingine hata mazingira ya nyumbani.

Kaka Mkuu huwa ni kijana anayejitambua vizuri ambaye kwa hakika anaweza kuwasaidia walimu vizuri katika kuhakikisha shule inafanya mambo yake vizuri bila shida yoyote ile. Katika mazingira fulani kaka mkuu anaweza hata akaombwa na walimu kuwasaidia kuwatafutia makaazi ya kupanga kwa walimu wapya shuleni hapo.

Kaka mkuu huwa mara nyingine na urafiki na walimu kadhaa na hata ukitaka kuzifahamu siri za walimu fulani Fulani na hata siri za shule basi kaka mkuu huwa ni mtu sahihi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.