Habari za Punde

Majaribio ya Vijana wa Mchezo wa Mpira wa Kikapu Zanzibar Yaliosimamiwa na Refocus Africa Yafikia Tamati.

Baadhi ya Wachezaji wa mpira wa Kikapu Zanzibar walioshiriki katika mazoezi ya majaribio  yalioandaliwa na Refocus Africa yaliofanyika katika uwanja wa Mao Zedung Zanzibar.  


Tumemaliza majaribio yetu salama na tulifanikiwa kupata wachezaji wazuri wengi ila kwa bahati mbaya tulikosa height waliyoitaka.

Kitu kizuri ndani ya hili, Refocus Africa wameahidi kurudi na kupunguza vigezo hasa cha kiko ila wanataka kuwaona vijana wamebadilika viwango. Kusimamia hilo wameomba mambo yafuatayo;

1. Vijana wabaki vile vile katika form ya Academy ambapo wizara yetu imeliridhia hilo na kuhusu kutumia uwanja wa Mao kwa mazoezi kwa siku watakazopangiwa.

2. Idadi ya vijana iongezeke hasa wenye umri mdogo wa miaka 10 - 16.

3. kuwe na mashindano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yatarekodiwa na kutumwa kwenye website ya Academy ili yaonekanwe dunia nzima

4. Vijana wapate proper training kutoka kwa wataalamu.

Refocus Africa kwa kushiririkiana na wizara chini ya office ya commissioner wataweka gym maalum kwa ajili ya vijana hawa na kuleta mtaalam maalum kutoka Marekani ili awafundishe trainers wa hapa kwetu juu ya mazoezi maalum ya basketball. 

Vile vile muda wowote kuanzia January wataleta wakufunzi kutoka NBA kwa ajili ya kufanya mafunzo kwa makocha wetu hapa na kupatiwa vyeti.

Refocus Afrika tayari washatia saini mkataba maalum wa miaka miwili na kumuahidi Mheshimiwa Rais ndani ya kipindi hicho watahakikisha mchezaji japo mmoja kutoka Zanzibar atachezea NBA.

Nawashukuru wote kwa michango yenu juu ya hili na naomba tusisite kuitikia wito wa kujenga basketball yetu. 

Basketball ya Zanzibar itajengwa na wanabasketball wenyewe. 

Ahsanteni sana

Abdalla Juma Abdalla 

Katibu kamati ya muda BAZA






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.