Habari za Punde

Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ashiriki ujenzi wa maskani ya CCM Shengejuu, akabidhi misaada


MBUNGE wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba, pia ni Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande, akiweka tufali katika ujenzi wa maskani ya CCM Shengejuu, ujenzi huo umefanywa na vijana wa UVCCM Zanzibar, wanaoshiriki Matembezi ya Kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
KIONGOZI wa Vijana wa UVCCM Zanzibar wanaoshiriki Matembezi ya kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar Asya Sharif Omar, pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba (kushoto) akimabidhi Mwenyekiti wa tawi la CCM Shengejuu Wilaya Wete, tawi hilo lililojengwa na Vijana hao kupitia ufadhili wa Mbunge wa Jimbo la Kojani Hamad Hassan Chande.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MBUNGE wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba, pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande, akizungumza na Vijana wa UVCCM Zanzibar walioshiriki katika Matembezi ya Kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya zanzibar, kabla ya kukabidhi msaada wa Maji, kulia ni Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Abdalla Juma Mabodi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MBUNGE wa Jimbo la Kojani pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande, akimkabidhi katuni 80 za Maji mkuu wa matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, hafla iliyofanyika skuli ya Sekondari Mchangamdogo Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.