Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi atoa salamu za rambirambi

                                                  STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

Pemba                                                                     03.01.2022


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Ramadhan Hamza Chande, Mwakilishi Mstaafu wa Jimbo la Jang’ombe, liliopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.


Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo pia, kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Bi Fatma Suleiman, Diwani Mstaafu wa Kwaalinato, Jimbo la Jang’ombe, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.


Katika salamu hizo za rambirambi,  Rais Dk. Mwinyi alieleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuzinasihi familia za marehemu hao kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.


Rais Dk. Mwinyi alimuomba Mwenyezi Mungu awalaze Marehemu wote mahala pema peponi,  Amin.


Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.