Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa Awasili Songea.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakisalimiana na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Songea kwa ziara, Januari 2, 2022. Kutoka kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini, Dkt. Damas  Ndumbaro, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Oddo Mwisho na wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (wa pili kushoto) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Meja Jenerali Wilbert Ibuge wakati alipowasilisha Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa huo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Songea kwa ziara mkoani Ruvuma,


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  Majaliwa (kulia) wakiagana na viongozi wa Wilaya ya Ruangwa kabla ya kuondoka wilayani humo kuelekea Songea kwa ziara Mkoani Ruvuma, Januari 2, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.