Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi azindua Jengo jipya la Mahkama Kuu ya Zanzibar Tunguu


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Viongozi wa Serikali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora.Mhe Haroun Ali Suleiman, Rais Mstaaf wa Zanzibar.Mhe Dk.Amani Karume, Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma na Jaji wa Mahkama ya Rufaa Tanzania.Mhe Omar Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya Jengo jipya la Mahkama Kuu Zanzibar Tungu, wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo hilo ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa kitambaa na Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan, kuashiria kulifungua Jengo jipya la Mahkama Kuu Zanzibar Tunguu, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kulifungua Jengo Jipya la Mahkama Kuu Zanzibar Tungu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukifu ya Zanzibar na (kulia kwa Rais) Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Ali Mohamed Shein,Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba.Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Sita Mhe.Dk.Amani Karume.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandisi wa Mahkama Kuu Zanzibar Eng.Mussa Ali Hamad, akitowa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahkama Kuu Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe,.Haroun Ali Suleiman, Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein na Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Sita Mhe.Dkt.Amani Karume.(Picha na Ikulu)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.