Habari za Punde

Uzinduzi wa Chaneli ya Elimu (EZTV) Skuli ya Kwarara

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya makaazi Mhe Riziki Pembe Juma  akiikagua chaneli ya Elimu Zanzibar  TV (EZTV) huko skuli ya Kwarara Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kuizindua  ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inafikia kilele chake kila ifikapo tarehe 12 Januari.
Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Khamis Juma katikati akizungumza baada ya uzinduzi wa   chaneli ya Elimu Zanzibar  TV (EZTV) huko skuli ya Kwarara Mkoa wa Mjini Magharib  ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inafikia kilele chake kila ifikapo tarehe 12 Januari.


 Na Rahima Mohamed      Maelezo      3/1/2022

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt. Hussein Ali Mwinyi imefanya jitihada kubwa ya kujenga miundombinu ya sayansi na teknolojia ili Zanzibar iendane na kasi hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya makaazi Mhe Riziki Pembe Juma  kwa niaba ya Waziri wa Nchi,Ofisi  ya Rais,Katiba,Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala wakati akizindua chaneli ya Elimu Zanzibar  TV (EZTV) huko skuli ya Kwarara Mkoa wa Mjini Magharib  ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inafikia kilele chake kila ifikapo tarehe 12 Januari.

Amesema jitihada za kuimarisha miundombinu ya teknolojia ikiwemo mkonga wa Taifa Nchi nzima ili kuimarisha na kurahisisha  mawasiliano kwa lengo la upatikanaji wa elimu nchini.

Aidha Waziri Riziki amewataka Wizara ya Elimu kuhakisha wanakipatia mahitaji yote ya msingi  kituo hicho ili kitumike kwa usahihi katika kujifunza na kutoa elimu  bora kwa wanafunzi kwa lengo la  kukuza mtaala wa elimu nchini.

Vilevile amesema Wizara ya  Elimu wanatakiwa  waandae mpango madhubuti  wa kuhakikisha wanazisaidia skuli zote zilizopo kuwekeza miundombinu ya Tehama ikiwemo tv ili wanafunzi wa skuli hizo  waweze kufaidika na televisheni hiyo.

Nae katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Khamis Juma amewataka watendaji wa televisheni hiyo kuwa wabunifu na kukitunza kituo hicho kwa lengo la kutoa huduma bora kwa jamii.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume  ya Utangazaji Zanzibar Suleiman Abdallah amewataka viongozi wa wizara hiyo wawasimamie watendaji wa kituo hicho  na wanafuata maadili ya utangazaji kwa kuhakikisha amani inadumu nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.