Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Aendelea na Ziara Yake Kisiwani Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na wananchi kulinda miundombinu inayojengwa na Serikali ili iweze kudumu kwa muda mrefu, akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba, kutembelea Miradi ya Maendeleo inayojengwa katika Mikoa Mitano ya Zanzibar Unguja na Pemba.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui wakati wa ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Kisiwani Pemba. kutembelea Miradi ya Ujenzi wa Hospitali za Wilaya.  

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi kulinda miundombinu inayojengwa na Serikali ili iweze kudumu kwa muda mrefu .

Mhe. Hemed ameyasema hayo wakati akikamilisha ziara ya Mikoa mitano ya Zanzibar ya kukagua Miradi ya maendeleo inayojengwa na Serikali kwa fedha za Mkopo wa kukabiliana na athari za ugonjwa Uviko 19 kutoka IMF Mkoa wa Kaskazin Pemba. 
 
Amesema ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha anakuwa Balozi wa kulinda Miundombinu hiyo ili idumu kwa muda mrefu na kuwafaa wananchi wa vizazi vijavyo. 
 
Amesema Serikali ina wajibu wa kujenga Miundombinu imara na ya kisasa inayoendana na wakati hali ambayo itapelekea upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi wa Zanzibar. 
 
Mhe. Hemed ameongeza kuwa ni vyema kwa wakandarasi hao kuzingatia muda wa kumaliza miradi hiyo na kuwataka kuongeza juhudi na kujiandaa kutosita kwa miradi hiyo kipindi cha Mvua kitakapofika.
 
Nae waziri wa Afya Ustawi wa Jamii wazee Jinsia na Watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amempongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuamua kukagua miradi hiyo na kueleza kuwa hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Matari Zahor Masoud amesema Serikali ya Mkoa imekuwa ikitembelea miradi hiyo ili kuona maendeleo yake na kuahidi kuendelea kutoa mashirikiano ya kutosha katika kukamilika kwa miradi hiyo.
 
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
13 Februari 2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.