Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji,
Viwanda, Biashara na Mazingira wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais, Dkt. Andrew Komba wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua
shughuli za kilimo msitu ya alizeti katika shamba darasa lililopo Kijiji cha
Haubi Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo Machi 12, 2022, kupitia
Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika
Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara
na Mazingira, Mhe. David Kihenzile akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kamati
hiyo kujionea shughuli ya utengaji wa msitu wa Intela wenye ukubwa wa hekta
863.4 kuwa hifadhi ya kijiji cha Haubi wilayani Kondoa mkoani Dodoma chini ya
Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika
Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ziara
iliyofanyika leo
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na
Mazingira wakiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua shughuli ya utengaji wa
msitu wa Intela wenye ukubwa wa hekta 863.4 kuwa hifadhi ya kijiji cha Haubi
wilayani Kondoa mkoani Dodoma chini ya Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika
na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa
na Ofisi ya Makamu wa Rais, ziara iliyofanyika leo
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji,
Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua
Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika
Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo Machi 12, 2022.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
No comments:
Post a Comment