Habari za Punde

ZRB yaagizwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato kuisaidia serikali

Baadhi ya Wafanyakazi waliyoshuhudiya Makabidhiano ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango,kutokana na Mabadiliko ya Baraza la Mapinduzi, huko Ukumbi wa Wizara hiyo Mjini Zanzibar.  

Waziri  wa Nchi,Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango Dk. Saada Salum Mkuya akizungumza na Watendaji wa Wizara hiyo katika hafla fupi ya makabidhiano ya Wizara baina yake na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Jamali Kassim Ali, huko Ukumbi wa Wizara Mjini Zanzibar. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –Ikulu Mhe. Jamal Kassim Ali akiwashukuru Wafanyakazi wa Wizara ya Nchi,Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango, katika hafla ya Makabidhiano ya Wizara hiyo, huko Ukumbi wa Wizara hiyo Mjini Zanzibar.  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –Ikulu Mhe. Jamal Kassim Ali , akimkabidhi Ofisi ,Waziri  wa Nchi,Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango Dk. Saada Salum Mkuya, kutokana na Mabadiliko ya Baraza la Mapinduzi, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Wizara hiyo Mjini Zanzibar.
 

(PICHA NA MARYAM KIDIKO / MAELEZO)

Na Kijakazi Abdalla            Maelezo  15/03/2022

Waziri  wa Nchi,Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango Dk. Saada Salum Mkuya ameziagiza taasisi zinazohusiana na ukusanyaji wa mapato ikiwemo ZRB kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.

Kauli hiyo ameitowa wakati akizungumza na watendaji wa Wizara hiyo katika hafla fupi ya makabidhiano ya Wizara baina yake na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Jamali Kassim Ali iliyofanyika katika Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango.

Amesema  serikali imekuwa inategemea mapato kutoka kwa walipa kodi ili kuweza kundesha nchi hivyo ni vyema kubuni mbinu mpya  ya kukusanya mapato.

Alisema miongoni mwa mambo ambayo serikali imekuwa inategemea kuleta maendeleo katika ukusanyaji wa mapato ni pamoja na ujenzi wa barabara,Ujenzi wa Skuli na huduma nyengine ambazo ni muhimu kwa jamii.

Kwa Upande wake Waziri aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Jamal Kassim Ali amewashukuru wafanyakazi wa wizara hiyo kwa mashirikiano waliyompa katika kipindi chote alichokuwepo hapo.

Aidha amewataka watendaji wa Wizara ya Fedha kufanya kazi kwa pamoja na kutumia ujuzi na uzoefu ambao itasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo ambayo serikali  inayategemea.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.