Habari za Punde

Agizo la Mhe.Rais Kutekelezwa --GEKUL

 
Na.Adeladius Makwega-WUSM

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Pauline Gekul ameliambia Bunge kuwa Serikali itakarabati viwanja saba vya michezo nchini kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na imetengwa bilioni 10 kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Gekul amesema hayo Bungeni Mei 24, 2022 akijibu maswali kadhaa yaliyouliza kwa wizara yake, likiwamo swali la mheshimiwa Festus Sanga Mbunge wa Makete likiwa swali la nyongeza lililochagizwa na maelekezo ya Naibu Spika Musa Zungu.

“Serikali inashirikiana na wadau mbalimbali kukarabati viwanja vya michezo nchini, wakiwamo Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao wana viwanja vingi nchini na mazungumzo yamekamilika, zoezi hilo litanyika mapema mwaka wa fedha unaokuja.”

Awali Naibu Waziri Gekul alilieleza bunge kuwa wizara yake imeshakamilisha hatua za awali za michoro ya Sports and Arts Arena ambapo ujenzi wote utagharimu shilingi bilioni 550/- kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Huku vikao vya mashauriano baina ya wizara na mkoa wa Dar es salaam vinaendelea juu ya eneo la ujenzi la Luguruni lenye ukubwa wa ekari kumi na nusu ambalo ni eneo mojawapo pendekezwa tu kwa jiji la Dar es Salaam.

Wakati Bunge likiyapokea majibu ya maswali hayo kutoka kwa Naibu Waziri Gekul Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Mohammed Mchengerwa alishiriki kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.